Mwenyekiti wa umoja wa vijana UVCCM Mkoa wa Dsm Atoa Pongezi Kwa Vijana Wa Chamazi

Mwenyeki wa Uvccm Mkoa wa Dar es Salaam Ndg Musa Kilakala akitoa pongezi siku ya jana Dec 03 kwa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi kata ya chamazi msufini kwa kuanzia michuano ya Rede Cup 2017 kwenye uwanja wa shule ya msing chamazi alipo kuwa mgeni rasmi kwenye fainali ya michuano ya Rede Cup 2017.
Nukuu : "Nimefurahi sana leo hii kuwa hapa na kujumuhika na nyinyi nawapongeza sana vijana wa chamazi kwa kuwa na utulivu,upendo na ushirikiano mpaka leo hii najua ni changamoto nying mmepitia mpaka kufika hapa,nawapongeza sana tena sana" pia Ndg Musa Kilakala ametoa wito kwa vijana wa mkoa wa Dar es salaam kuipenda michezo,na kuifanya kuwa ajira kwao pia waitumie michezo kuwaweka pamoja na kushirikiana bira ubaguzi wa rangi, dini wala jinsia. 

Maoni