MZAMBARAUNI,KISEWE NADHANI WANATUJUA SISI KWETU NI USHINDI

Kuelekea kwenye mchezo wa kirafiki wa REDE kati ya MZAMBARAUNI QUEENS na KISEWE QUEEN utakao chezewa kwenye uwanja wa mzambaruni siku ya jumapili. Meneja wa team iyo Ndg Muhunzi na team captain wa team iyo wapata fursa ya kuzungumzia maandalizi yao.

Muhunzi "Tumejianda vizuri,tunacheza nyumbani na sifa ya kucheza nyumbani ni ushindi tu.

SR.. swali kitu ngani kinakufanya ujiamini sana?

Muhunzi: "Najiamini kwa sababu ya maandalizi mazuri ya vijana wangu pia ninawachezaji wenye uwezo mkubwa ukimwangalia kama SARA ni moja kati ya wachezaji wanao ogopeka sana kwa kuwa na kiwango kizuri,na Kisewe Queens tulishawai kucheza nao na tuliwafunga goal 3 kwa 0 ivyo tunawafahamu namna wanavyo cheza,japo si team ya kuibeza sana ila naipa nafsi kubwa team yangu ya MZAMBARAUNI kuibuka na ushindi siku iyo.

SR..swali ni mchezaji ngan unamwofia sana kwenye team pinzania

Muhunzi:"Kuna wachezaji watatu (tina) na wale mapacha wawili (neema na rehema) nawaofia sana kwa sababu ni wachezaji wazuri wanajituma sana rakini
, naamini vijana wangu watapambana na wataibuka na ushindi na kuwapa molali nimewaahidi vijana wangu kama watafanya vizuri kwenye mchezo huu wa jumapili nitawapatia zawadi kubwa sana kwa sasa siwezi kusema ni zawadi ngan rakini ni kubwa sana"

Huyo wa mbele mwenye kilemba cha njano ndio Sara (tall) team captain wa Mzambarauni.

Sara Captaini: "Mazoezi yanaendelea vizuri na tumejianda vizuri kwa mchezo wa jumapili.

SR..swali unadhani unaweza kuwafunga kisewe

Sara Captain: "Ndio tutawafunga,maana ata mchezo wa kwanza tuliwafunga kama unakumbuka goal 3 kwa 0,wanatujua vizuri sisi sio watu wa mchezo mchezo kabisa"

SR..swali vip unaamini uchawi kwenye michezo?

Sara Captain: "Uchawi upo rakini sisi hatupi nafasi kabisa tunaamini uwezo wetu"

Maoni