Ngassa sasa rasmi Ndanda Fc

Aliyekuwa mchezaji vilabu vya Yanga, Azam, Simba na Mbeya City, Mrisho Ngassa ameungana na Kikosi cha Ndanda FC walioweka kambi Mbeya kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa FA kesho vs Boma FC.

Ngassa amesaini mkataba wa mwaka mmoja kuichezea Ndanda FC baada ya kumaliza mkataba wake na Mbeya City.
Ngassa ambaye alijiunga na Mbeya city mwaka mmoja uliopita akitoka klabu ya Fanja fc ya Nchini Omani ameondoka Mbeya City kutokana na kutokuonyesha kiwango bora jambo lilimfanya kukosa namba katika kikosi cha kwanza cha klabu hiyo licha ya nafasi kadhaa ambazo amekua akipea katika kikosi hicho.

Maoni