Shukrani kwa wasomaji wetu

Neno shukrani lina nguvu linapotamkwa kwa yule aliyefanya jambo, unaposema asante au nashukuru unaumba nafasi ndani yake yule uliyemshukuru aendelee kukutendea mema. Unapomshukuru yule aliyekutendea jambo jema unakuwa umewasha moto ndani yake, utakao kuwa ukimsukuma aendelee kukusaidia tu hata kama hana vitu vingi au mali nyingi.

Na sisi tunasema Asant na Tunawashukuru wasomaji wetu kwa kuwa pamoja nasi kwa mwaka huu wa 2017… Ni imani yetu kuwa tutaendelea kuwa pamoja kwa mwaka ujao wa 2018.

Katika mwaka ujao wa 2018 tumepanga kufanya maboresho kadhaa kwenye blog yetu yatakayoendelea kukupatia ladha maalumu na yenye upekee kwenye habari na taarifa zetu. Aidha, ushauri, maoni, mapendekezo na ukosoaji wako ni muhimu sana katika kukuletea kitu bora zaidi tupe maoni yako kwa kutuandia sms kwa namba 0629631116 au 0689232546  Ahsante sana.

Pia tunapenda kuomba radhi kama kuna mtu tulimkera kwa namna moja ama vingne kwenye habari au taaarifa yeyote ilio lipotiwa kwenye blog hii.

… Endelea kuwa msomaji wetu, endelea kuhabarika na shabanirapwiblogsport. com.

Maoni