UMUHIMU WA MAZOEZI

Mazoezi yana faida nyingi na kubwa sana kiafya. Watu wengi wanaofanya mazoezi wanakuwa na afya nzuri na huishi vizuri kuliko watu wasiofanya mazoezi. Umuhimu wa mazoezi ni pamoja na
1. Husaidia kujenga mwili – Ukitaka kuujenga mwili wako vizuri basi fanya mazoezi ya kujenga mwili
2. Husaidia kuongeza kinga ya mwili – Watu wanaofanya sana mazoezi huwa na kinga nzuri ya mwili na hawaumwi ovyo magonjwa ambayo watu wa kawaida huugua mara kwa mara
3. Husaidia kudhibiti uzito wa mwili
4. Ni kinga kubwa na imara sana dhidi ya magonjwa yasiyoambukizwa – Mazoezi husaidia sana kuzuia na kudhibiti kisukari, presha, magonjwa ya moyo na mfumo wa damu na msongo. Fanya mazoezi ili kujikinga dhidi ya kisukari, shinikizo kubwa la damu (presha), uzito mkubwa uliopitiliza (obesity), msongo na magonjwa ya moyo na mfumo wa damu. Kama tayari unaumwa hayo magonjwa basi fanya mazoezi ya kutosha ili kuyadhibiti vizuri na kuishi vizuri kabisa huku ukizingatia matibabu
5. Husaidia kuunguza na kuondoa kiasi cha chakula na mafuta kilichozidi mwilini – Kila kitukikizidi kina madhara mwilini, kadhalika na chakula na mafuta. Fanya mazoezi ili kuondoa mafuta yaliyozidi na chakula kilichozidi
6. Husaidia kuondoa manyama uzembe, vitambi kwa akina baba na matumbo makubwa kwa akina mama – Huhitaji kutumia tiba za bei kubwa. Fanya mazoezi ya kupunguza mwili, kitambi na manyama uzembe kisha utafanikiwa bila gharama kubwa
7. Husaidia kuufanya mwili kuwa mwepesi na rahisi kukabiliana na dharura yoyote – Mtu mwenye mwili wa mazoezi huweza kukimbia, kuruka na hata kujiokoa kwa urahisi zaidi kuliko mtu asiyefanya mazoezi.

Maoni