UVCCM CHAMAZI KUMUUNGA MKONO JPM

Katika kuunga mkono harakati za Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk John pombe magufuli kuweka mazingira katika hali iliyo safi na usalama Umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi kata ya chamazi kwa kushirikiana na viongozi wa serikali za mtaa, wamekuwa na utaratibu wa kufanya usafi kila jumamoss katika maeneo mbalimbali ya kata  ya chamazi, na jumamoss hii ya tarehe 23.12.2017 zoezi ilo litaendelea kataka eneo la Kiponza.

Kutoka kwa katibu hamasa na chipukizi Ndg Najim Nyanza amesema "Zoezi ili ni la kila mmoja na si wanaUVCCM pekee ivyo wananch wa Kiponza wajitokeze kwa wingi na kushirikiana nasi katika zoezi ili" amesema Nyanza. 

Naye Mwenyekiti wa UVCCM Ndgu Nasri Mkalipa amesema "Umoja wa vijana wa ccm kata ya chamazi  tumedhamiria kuifanya chamazi kuwa safi,na  utaratibu wa kufanya usafi katika kata yetu umeanza toka Desemba mwaka jana ivyo tunaendelea na tutazidi kuendelea sisi kila jumamoss ni usafi"

na hii ni mara baada ya uzinduzi uliofanywa na Rais wa jamhuri ya muunano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli kwa kuagiza kila Halmashauri nchini kufanya usafi kwa kila jumamosi ya mwisho wa mwezi. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt . John Pombe Magufuli alipofanya usafi katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru tarehe 9 Desemba 2015.

Maoni