WAJIBU WA MUME KWA MKEWE.

..UKUMBUSHO...!!

Usimtolee maneno makali mkeo anapotaka kukwambia jambo.

itunze heshima yake ka yeye anavyotunza heshima yako.

Usijaribu kumuonesha kuchokwa na yeye uyaingiza huzuni na mawazo katika moyo wake.

Tunza familia yako kwa kutoa huduma zinazohitajika sio ukiingia ndani kama mwanajeshi uso umeukunja.

Maliza matamanio yako yote kwake usitafute wanawake wengine wa nje tone moja la manii linalotoka kwako kwenda kwa mkeo ni swadaqa usiibadilishe swadaqa hii kuwa ni madhambi.

Maana ya hadithi :Aliulizwa mtume ( s.a.w ) na maswahaba zake je hata mmoja wetu akimuingilia mkewe analipwa thawabu ?
Mtume ( s.a.w ) alijibu kwa kusema huoni tone hilo hilo akilichukua na kuliweka sehemu isiostahiki anapata dhambi.

Kuna watu hawawthamini wake zao hata kidogo mtu ni mzima na afya yake miezi mitatu hajampa mke wake haki yake anazunguka na Wanawake wa nje na kupoteza pesa.

Fahamu ujue ipo cku utakuja kupatwa na tatizo washindwe kukujali wote kisha utataka msaada kutoka kwa mke wako hali yakuwa nguvu umezipoteza kwa kuhudumikia wengine.

Unaposafiri mkeo unamuachia pesa haitoshelezi mahita yake na umemuacha na watoto wewe hata hujali.

Tambua kama ni nguvu ipo cku zitakwisha uje ujute wakati umeshapoteza mda ubakie kujuta.

Rudi kwa mola wako na umuombe msamaha kwa uliyoyafanya usimtese mkeo na heshima machozi yake.

Mtume ( s.a.w ) anasema miongoni mwa watu watatu ambao dua zao zinajibiwa mara moja ni mtu aliye dhulumiwa una mdhulumu mkeo kwa kujali wengine umemchukua kwao mtoto mwari kisha unamtesa.

HUU UJUMBE UMFIKIE KILA MWANAUME ALIE OA NA ANAPUUZA WAJIBU WAKE KWA MKEWE.

Maoni