WAKULIMA WA VIAZI MVIRINGO MKOANI NJOMBE WALIA NA LUMBESA

Wakulima wa viazi mviringo kutoka vijiji 4 vya kata ya luponde wilayani njombe wameiomba serikali kupitia wakala wa vipimo kuanzisha vituo vya Kuuzia mazao kwa kutumia vipimo vya mizani ili kuepukana na hali ya unyonyaji inayofanywa na madalali wanaofungasha kwa mfumo wa lumbesa.
Wakizungumza na Kituo hiki wakulima wa kata ya Luponde wamesema kuwa endapo kukiwa na vituo kwa ajili ya kuuza mazao kwa pamoja katika vijiji itasaidia kudhibiti lumbesa huku wakiitaka serikali kusimamia zaidi vipimo vya uzito usiozidi kilo miamoja kwa kuwa na mizani kila kituo kwenye vijiji badala ya wafanyabiashara kununua mazao mashambani kama ilivyo hivi sasa.



Chanzo : Greenfm Tanzania

Maoni