WAZALENDO QUEENS WASHINDI WA REDE CUP 2017 CHAMAZI

Mashindano ya Rede Cup yalio andaliwa na kusimamiwa na Ummoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi kata ya chamazi tawi la Msufini atimae jana Dec 03 yamefikia tamati kwa kuchezwa mchezo mmoja wa fainal ulio zikutanisha Wazalendo Queens na Team Kujiamini na team ya Wazalendo Queens kuibuka washindi wa Mashindano ayo na kujipatia kitita cha fedha cha sh 10,0000 na uku washindi wa pili Team Kujiamini nao wakijipatia kitita cha sh elf 70000 na uku washindi wa tatu  Super Nyota wakaibuka na kitita cha sh elf 50000,mgeni rasmi wa fainal iyo alikuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es Salaam Ndg Musa Kilakala na kabla ya kuanza kwa mchezo uwo wa fainal mgeni rasm alitoa vyeti vya heshima kwa waandaji wa michuano iyo ya REDE CUP 2017 walio pata vyeti ivyo vya heshima ni

Nasri Bakari Mkaripa (Mwenyekiti)

Juma Bega Zonzo (katibu)

Najim Nurdin Nyanza (katibu    hamasa na chipukizi)

Muhunzi ally (M/kiti wa idara ya burudani na michezo)

Ibrahim Bofu (katibu wa idara ya michezo)

Na baadhi ya viongozi wa matawi

Baada ya kukabidhi vyeti ivyo vya heshima kwa waandaji wa michuano iyo mgeni rasmi aliwapongeza vijana wa chamazi kupitia chama cha mapinduzi kwa kuipenda michezo na kuwa mfano bora na wa kuingwa kwa kata,mkoa na taifa kwa ujumla.

Maoni