APANGALO MUNGU HALINA MAKOSA, POLENI SANA WANACHAMA WA UVCCM TAWI LA KISEWE - NASRI MKALIPA.


Jumanne 30 January 2018.

Maneno hayo yalisemwa Jana na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Kata ya Chamazi Ndg. NASRI MKALIPA alipowatembelea kwa ajili ya kuwajulia hali wanachama wa UVCCM Tawi la KISEWE. Wanachama hao watano wanasumbuliwa na homa sambamba na miguu kuuma.

"Nilipopigiwa simu na Mwenyekiti wenu wa Vijana wa Tawi hili kuwa kuna Vijana watano wanaumwa kwa wakati mmoja nilipata mstuko, hapo hapo nikaacha nilichokuwa nakifanya ili kuja kuwatazama na kuwajulia hali" alisema MKALIPA.

"Yote haya yanakuja kwa kuwa Mimi ni muumini mzuri wa asili ya CCM ya WATU na HAKI, imani yangu imejikita katika hivyo viwili kwa hiyo bila nyinyi hakuna maana ya Mimi kuwa kiongozi nawaahidi kuwa na nyinyi katika KIPINDI CHA SHIDA NA RAHA" alisema MKALIPA.

" Nawaombea kwa Mungu mpate nafuu haraka ili muweze kuendelea na ujenzi wa Taifa na Chama Cha Mapinduzi kiujumla" alisema MKALIPA.

Pia Ndg. MKALIPA alijumuika na familia za wagonjwa hao na kupata chakula cha Mchana nyumbani kwa mmoja wa wagonjwa hao. MSINGI WA CCM NI HAKI NA WATU.

#DSM HatubebiMabegi. #TukutaneKazini.

Maoni