CHAMAZI, KUNDUCHI KUMUUNGA MKONO RAIS MAGUFULI

Jumapili 28 January 2018.

Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Kata ya Chamazi JANA Jumamosi  waliungana na UVCCM Kata ya Kunduchi kuunga mkono agizo la kufanya usafi alilolitoa  Rais wa Tanzania Mh. JOHN POMBE MAGUFULI ambapo mgeni Rasmi alikuwa Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Dar es Salaam Ndg. MUSA KILAKALA.

Usafi huo uliohusisha maeneo ya Zahanati ya Tegeta, Kituo Cha Polisi Tegeta na Soko la Tegeta ulihudhuriwa na wanachama pamoja na viongozi wa UVCCM wa Ngazi ya Mkoa Wilaya na Kata za jiji la Dar es Salaam.

NUKUU YA LEO.

"Siku Vijana wa CCM mkijipambanua kwa Umoja wenu Chama kitawapa nafasi, lakini mkijipambanua kwa chuki na uhasama mtabaki wasindikizaji tu wa wengine" KHERI JAMES. Mwenyekiti UVCCM Taifa.

Sisi Vijana wa KATA YA CHAMAZI Tunakuunga mkono Mwenyekiti wa UVVCM Taifa KWA VITENDO na Tunasema TUTASEMA KWELI DAIMA, UNAFIKI KWETU NI MWIKO.

#HatubebiMabegi.
#TukutaneKazini.

Imetolewa na
Idara ya Hamasa na Chipukizi
Kata ya CHAMAZI.

Maoni