ENG LUCAS MASHAURI ATIMIZA AHADI YAKE KWA SHULE YA MSINGI JUHUDI

Na Comrade Sambala

Eng Lucas Mashauri leo ametimiza ahadi yake kwa shule ya Msingi Juhudi iliyopo manisipaa ya Temeke Jijini Dsm ahadi aliyoitoa mwaka jana mwezi dec alipoalikwa Mgeni Rasmi kwenye Mahafali ya Darasa la saba.

Katika halfa ya  wazazi ya kukabidhi zawadi kwa wanafunzi waliofanya Vizuri  iliyofanyika shuleni hapo leo jumapili tarehe 28 Eng Mashauri amekabidhi Mifuko 100 ya Saruji Matofali 1000 malaori mawili ya Mchanga pamoja na fedha taslimu Tsh 1,000,000

Mbali na kukabidhi vitu hivyo pia amasema ataendelea kuunga mkono jitihada za maendeleo kokote Tanzania na kuwataka na wadau wengine kufanya hivyo.

Vile vile Eng Mashauri amemwomba mkuu wa Mkoa wa DSM Paul Makonda katika jitihada zake za kujenga ofisi na madara basi aiweke mbele shule ya msingi Juhudi sababu wao wameshaanza kuonyesha utayari wa kuunga mkono jitihada zake.

Nao uongozi wa Shule ya msingi Juhudi wamemtunuku cheti cha Shukurani katika kutambua jitihada zake katika mendeleo ya Kata ya Kiburugwa na Manispaa ya Temeke kwa ujumla.

Vitu hivyo vyote vimekabidhiwa kwa Wakilishi wa mkurugenzi Manispaa ya Temeke ambaye ni Afisa Elimu Ufundi na Ujenzi ndugu Salum Upunda leo mchana katika eneo la shule ya Msingi Juhudi Kata ya Kiburugwa.

Maoni