HII NDIO MAANA YA HATUBEBI MABEGI

HATUBEBI MABEGI kwa sasa ndio ndio kauli mbiu ya Mkoa wa Dar es Salaam ambayo imetangzwa rasmi na Mwenyekiti Uvccm Mkoa wa Dar es Salaam Ndg Musa Kilakala. 

Neno hili limeasisiwa na UVCCM KATA YA CHAMAZI likiwa na maana ifuatayo:

Kila kiongozi wa UVCCM inabidi awe na uthubutu sambamba na kufanya kazi kwa bidii bila uvivu (kutokana na kubeba begi) katika eneo lake la utawala sambamba na kushirikiana na viongozi husika wa maeneo yao kama Mbunge, Diwani, Mwenyekiti wa Mtaa n.k.

Lengo kuu ni kuhakikisha Kijana anakuwa na sauti na kuweza kusema panapohitajika kusema, kutatua matatizo ya jamii kwa haraka na kuitikia wito anapoitwa na wananchi, viongozi wa ngazi ya chini    yake, ngazi yake na juu yake kwa haraka hususani katika eneo lake la utawala.

Kwa maana unapofanya kazi katika eneo lako la utawala ndipo unapoweza kutatua shida za wananchi na hapo kauli yetu ya #SibebiMabegi utakuwa umeitendea haki sambamba na kauli ya Taifa ya #TukutaneKazini.

Kwa maana ukiwa unatimiza wajibu wako kikamilifu tena kwa wakati nina imani Mara nyingi utakuwa kazini ukitatua kero za wananchi ama mwenyewe ama kwa kushirikiana na viongozi wa nafasi ya chini yako, ngazi yako au ya juu yako kama Wenyeviti wa Serikali ya Mtaa, Madiwani, Wabunge na Mawaziri.

Kwa hiyo naomba vijana wote kuiunga mkono kauli hii ya #TusibebeMabegi kwani itasaidia kutufanya tuwe wepesi wa kutekeleza majukumu yetu na tunayopewa na viongozi kwa haraka na hatimaye kutatua changamoto za wananchi na hatimaye Chama Cha Mapinduzi kuaminika zaidi na wananchi na kuendelea KUSHIKA DOLA.

#HatubebiMabegi.
#TukutaneKazini.

Imetolewa na
Nasri Mkalipa
Mwenyekiti UVCCM Chamazi.

Maoni