HIKI NDIO CHANZO,DALILI NA MATIBABU YA MWANAUME KUMWAGA MBEGU KIDOGO.

mbegu kidogo ni zipi?
kwa kawaida mil moja au cc moja ya mbegu za kiume inatakiwa kua na mbegu million 20 na zaidi, mwanaume ambaye anatoa mbegu chini ya milioni 15 kwa kila cc huyo anahesabika ana upungufu mkubwa kiasi cha mbegu.
                                                       

kua na mbegu kidogo kuliko kawaida kunapunguza uwezekano wa mwanaume kumpa mimba mwanamke, japokua wakati mwingine unaweza kubahatisha na kumpa mimba mwanamke.

dalili za kua na mbegu kidogo ni zipi?
mara nyingi dalili kuu ni kushindwa kumpa mwanamke mimba, dalili zingine huweza kuja na kuonekana kulingana na chanzo husika kilichokufanya wewe mbegu zako zipungue lakini wingi wa manii unazomwaga haimaanishi na mbegu ni nyingi.
unaweza kumwaga kikombe kizima lakini ukipimwa hakuna hata mbegu moja iliyotoka.

sababu za mbegu kutolewa kidogo nini?
kemikali za viwandani; 
baadhi ya kemikali za viwandani tunazokutana nazo kutokana na mazingira tunayoishi na kazi tunazofanya huweza kusababisha mtu kuwa na kiwango kidogo sana cha mbegu...mfano kemikali za benzene, xylene,herbicides, dawa za kuua wadudu, dawa za kuua magugu shambani zote hizo zinahusika.
mionzi; mionzi kama ya x ray hupunguza wingi wa mbegu kutoakana na mara ngapi mionzi hii inakupata, kuendelea kupigwa mwanga kwa muda mrefu huweza kusababisha kupungua kabisa kwa kiwango cha mbegu kinachotolewa na muhusika.
joto sana kwenye korodani: mazingira yeyote ambayo yanachangia kiwango kikubwa cha joto kwenye korodani hupunguza kiwango cha mbegu,,,mfano kutumia laptop mapajani, kuvaa nguo nzito muda mwingi, kuoga na kukaa kwenye sink kubwa za maji ya moto, kuvaa tight zinazobana korodani kwenye mapaja na kadhalika.
kupiga punyeto; tabia za kupiga punyeto mara kwa mara hufanya kiwango cha mbegu kua chini sana kwani baadhi ya mbegu hutoka hata kabla hazijakomaa..hili ni tatizo kubwa kwa vijana wengi ambao wako kwenye umri wa kutafuta watoto.
matumizi ya dawa;
dawa aina ya anabolic steroids zinazotumika kujaza miili ya watu wanaofanya mazoezi ina tabia ya kupunguza ukubwa wa korodani na kusababisha kupungua utengenezaji wa mbegu lakini pia dawa za kulevya kama coacaine na bangi pia hupunguza ubora wa mbegu za kiume.
unywaji wa pombe na sigara; unywaji wa pombe kwa kiasi kikubwa unapunguza kiwango cha homoni za kiume kitaalamu kama testosterone ambazo huhusika kwenye utengenezaji wa mbegu pia sigara hupunguza kiwangi cha utengenezaji wa mbegu.
msongo mkali wa mawazo; msongo wa mawazo unaweza kufanya kuharibika kwa kiwango cha homoni mwilini, lakini pia mwanaume ambaye ana tatizo hili mawazo yake pia humfanya tatizo liwe kali zaidi,
unene; kiwango kikubwa cha unene huingilia utoaji wa mbegu kwa kuharibu mfumo mzima wa homoni zinazohusika na utoaju wa mbegu.
magonjwa mbalimbali ya mwili; magonjwa kama varicosele,magonjwa ya korodani, magonjwa ya zinaa kama gono, saratani za korodani, korodani ambazo hazijashuka chini vizuri, kuziba kwa mirija ya mbegu, matatizo ya njia za mbegu za kiume,baadhi ya magonjwa ya utumbo mkubwa huweza kusababisha ugumba.

 vipimo 
utrasound; kipimo cha utrasound hutumika sehemu mbalimbali kuangalia sehemu mbalimbali za korodani ikiwemo mirija kama iko sawa.
kiwango cha homoni; upimaji wa kiwango cha homoni mara nyingi hujaribu kuangalia kama kiwango cha homoni ya testosterone uko sawa.
post ejeculation analysis; kiwango kikubwa cha mbegu kwenye mkojo mara nyingi humaanisha kwamba mbegu zinatoka kwenye mirija na kwenda kuangukia kwenye kibofu cha mkojo badala ya kutoka nje kwenye uume.
genetic test; kipimo cha damu kwenye maabara zilizoendelea huweza kuonyesha matatizo ya kurithi au ya kuzaliwa nayo ambayo huweza kuathiri utoaji wa mbegu za kiume mfano tatizo la klenfelter syndrome.
ant sperm antibody test; kipimo hiki hupima aina ya askari wa mwili ambao hugeuka na kushambulia mbegu za mwanume kwa kudhani kwamba mbegu hizo ni adui kwa mwili.
sperm function test; kipimo hiki huangalia kama mbegu zinazotolewa na mwanaume zina kasi ya kutosha, ubora wa kutosha na muda gani zinaweza kuishi bila kufa baada ya kutoka nje ya korodani.
testicular biopsy; kipimo hiki hutumika kuchukua na kukata sehemu ya korodani na kuzipima kama utengenezaji wa mbegu uko sawa.

matibabu;
mara nyingi matibabu ya upungufu wa kiasi cha mbegu hutegemea zaidi chanzo husika cha tatizo, kama madaktari wakiweza kutambua chanzo au mgonjwa mwenyewe akiweza kutambua chanzo na kukiepuka basi anaweza akapata nafuu.
mfano wa matibabu hayo ni kama ifuatavyo.

kuepukana na vyanzo vya tatizo; kama umekutwa na tatizo hili ni vizuri ukaachana na utumiaji wa madawa au ulevi, mfano pombe, sigara, madawa ya kulevya, kupiga punyeto,kukaa mbali na mionzi na madawa mbalimbali ya wanyama na mimea.

upasuaji; magonjwa yote ambayo yanahusiana na kuziba kwa mirija, kuvimba kwa korodani, saratani za korodani, au varicose veins hutakiwa kufanyiwa upasuaji ili kuweza kulitatua tatizo.

matatizo ya tendo la ndoa; kwa wanaume ambao wanashindwa kusimamisha uume wakati wa tendo la ndoa ni vema wakatibiwa ili kuweza kuhimili tendo hilo na kutoa mbegu za kutosha.

matibabu ya homoni; baada ya vipimo vya homoni kama kuna ambazo zitaonekana zimepungua basi unaweza ukatibiwa kwa kupewa zile ambazo zimepungua.

kutibu magonjwa husika; magonjwa ya zinaa na mengine ambayo yanaonekana kushambulia njia ya uzazi na korodan zenyewe yanatakiwa yatibiwe.

fanya ngono siku hatari za mwanamke: kwa wale ambao mnatafuta mtoto ni vema ujifunza hesabu za siku za hatari ili mshiriki tendo siku hizo tu kwani mbegu za mwanaume zitakua kidogo zimekomaa na kuweza kumpa mwanamke mimba.

epuka vilainishi; baadhi ya vilainishi kama k-y gel, losheni na mafuta huweza kuzuia kasi ya mbegu za kiume hivyo jitahidi kutovitumia ili kujiweka salama wakati wa tendo la ndoa.

matumizi ya virutubisho; kuna virutubisho mbalimbali ambavyo hutumika sana kuongeza kiasi cha mbegu za mwanaume, binafsi nimeona ambavyo vimewasaidia ambao walikua na shida kama hizo..kwa dozi ya miezi mitatu mpaka sita mbegu huanza kuongezeka kama hakuna tatizo kubwa.
ukihitaji virutubisho hivi tuwasiliane.


mwisho; baadhi ya matatizo ya kutoa mbegu kidogo yanaweza yasitibike kabisa hata kwa kwenda kwenye hospitali kubwa sana, hivyo mgonjwa ni vizuri akubaliane na hali na ajue jinsi gani anaweza kuishi bila watoto au kulea watoto wa watu wengine.

Maoni