HOSPITALI YA MRARA BABATI HAIJWAHI KUTOKEA KIFO CHA MAMA MJAMZITO

Hospitali ya wilaya Babati MRARA
Mkoani Manyara imefikisha miaka miwili tangu kuanza kwake kutoa huduma ya afya ya uzazi katika hospitali hiyo kwa mafanikio makubwa bila ya kutokea kifo chochote kwa akina mama wakati wa kujifungua.
Mganga Mfawidhi wa hospitali ya MRARA Nikodemus Gaudence ameimabia WALTER HABARI kuwa hospitali hiyo imezidi kufanya kazi zake kwa umakini mkubwa ili kuepuka vifo vinavyotokana na uzembe.
Alisema ‘tangu kuanza kutolewa kwa huduma ya wazazi katika hospitali hiyo kwa takribani miwili sasa haijawahi kutokea vifo vya akina mama waliojifungua hospitalini hapa’.
Dk Nickodemus ametoa rai kwa kina mama kuhakikisha kuwa wanajifungulia katika vituo vya afya vilivyopo karibu ili kuepuka matatizo ya kiafya yanayotokana na kujifungua kienyeji.
Pamoja na hayo amewataka Wananchi kuwa na tabia za kupima
afya zao mara kwa mara ili kuweza kuepuka vifo visivyokuwa vya lazima.
‘ Ameeleza kuwa wengi wamekuwa wakipoteza maisha kutokana na kukaa na ugonjwa mwilini muda mrefu bila kupima hivyo anapokuja kugundua kuwa ni mgonjwa tayari ugonjwa unakuwa umefikia hatua mbaya zaidi.
Ameendelea kueleza kuwa kwa sasa Hospitali ya mji wa Babati Mrara ina vitengo mbali mbali kama,huduma ya kliniki kwa mama na mtoto,inawahudumia wenye magonjwa ya kifua kikuyu bila malipo,huduma ya macho,kitengo cha huduma ya magonjwa ya Akili,Ushauri Nasaha kwa wanaoishi na Virusi vya Ukimwi.
Aidha amesema Serikali inaendelea kuonyesha ushirikiano kwa kuendelea kutoa vifaa muhimu vinavyohitajika hospitali ili wananchi wapate huduma bora zenye kukidhi haja ya magonjwa ya wananchi.
Kuhusu wagonjwa wenye kadi za Bima ya afya na wasio na Bima Dk Nikodemus ameeleza kuwa huduma zinatolewa bila ubaguzi kwa watu wote.

Maoni