JOKATE MWEGELO ASHIRIKI KWENYE UFUNGUZI WA MASHINDANO YA REDE CHAMAZI.

Kaimu Katibu Hamasa na Chipukizi UVCCM Taifa Ndg. Jokate Mwagelo alipokuwa akifungua Mashindano ya Uvccm Chamazi Rede Cup 2018 jana Jan 06 katika uwanja wa Shule ya Msingi Chamazi Jijini Dar es Salaamu.

Jokate Mwegelo alisema anatumaini kuwa Kata zingine zitaiga mazuri yanayofanywa na UVCCM kata ya chamazi. "Nimefurahi kuona viongozi wa UVCCM Kata ya Chamazi wakiwa wabunifu kila Siku iendayo kwa Mungu,jambo hili walilolifanya ni kubwa sana,tuwapigie makofi" alisema Jokate Mwegelo

Kwa upande wake Mwenyekiti UVCCM. Ndg. Nasri Mkali alimshukuru  Jokate Mwegelo kuwa mlezi wa Jumuiya ya Vijana Kata ya Chamazi na Jokate amekubali ombi la kuwa mlezi wa Kata ya Chamazi katika maswala yote yanayohusu maendeleo ya Chama Cha Mapinduzi Jumuiya ya vijana.

 "niseme kutokana na furaha niliyonayo nimewapenda sana wana Chamazi kwa hiyo kuanzia  Leo Mimi nitakuwa mlezi wa Jumuiya ya Vijana katika Kata hii" alisema Jokate

Maoni