JOKATE MWEGELO KIDOTI KUWA MGENI RASMI UFUNGUZI WA MASHINDANO YA UVCCM REDE CUP CHAMAZI.

JOKATE MWEGELO maarufu kama KIDOTI anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa mashindano ya UVCCM CHAMAZI REDE CUP 2018,Mwenyekiti wa uvccm kata ya chamazi,Nasri Mkalipa akizungumza na shabanirapwibogsport.com amesema Jokate Mwegelo ndiye atakayefungua mashindano hayo yatakayo shirikisha team zaidi ya 13 kutoka kwenye kata iyo.

Alizitaji baadh ya team  zitakazo shiriki mashindano hayo kuwa ni
Kisewe queens, Kiponza, Mzambalauni queens,Bamia, Dovya na Kwa mkongo.

Mkalipa amesema mashindano hayo yanatalajia kuanza ivi karibu baada ya ufunguzi wa hapo jumamosi

Naye Katibu hamasa na chipukizi, Najim Nyanza aomba wadau na mashirika mbalimbali yajitokeze kudhamini mashindano hayo ili kuyapa nguvu, Najim Nyanza alisema "Mashindano haya yahusu wanauvccm wa kata ya chamazi pekee,lengo letu ni kufanya mchezo wa rede unakuwa mkubwa asa kwenye kata ya chamazi, hivyo napenda kuwaomba wadau na wapenda michezo kwa ujumla kuja kutia nguvu mashindano aya kwa namna moja ama vingne"

Uku baadh ya wachezaji  na viongozi wa team mbalimbali wakitoa tambo za hapa na pale kuelekea kwenye mashindano ayo.

Akizungumza kwa niaba ya nahodha wa tim ya KWA MKONGO, Amina Mohamedi alisema tunaingia kwenye mashindano haya kuchukua ubingwa na siyo kushiriki, maneno ambayo ni sawa na nahodha msaidizi wa KISEWE QUEENS Tina ambaye alisisitiza kuwa ubingwa ndiyo kipaumbele chao.

Maoni