Kanisa linalobatiza watu kwa Pombe laibuka Afrika Kusini, lapata Waumini 500 kwa miezi miwili


Bara la Afrika limebarikiwa kuwa na makanisa mengi ambayo yanashikilia msimamo na imani tofauti. Wengi wa wahubiri katika makanisa mengi hutumia maneno na kuhubiri maneno yenye kuvutia watu ambapo wengine hutumia mbinu mbalimbali kujizolea waumini

> Nchini Afrika Kusini ameibuka Askofu mmoja anayejulikana kwa majina ya Tsietsi Makiti ambaye amegonga vichwa vya habari kwa kutumia Pombe(Vilevi) kama msingi mkuu wa mahubiri yake. Askofu Makiti anahubiri kuwa Walevi wengi ambao wanapigwa vita na makanisa mengine ni lazima wavutwe kuingia makanisani

> Kanisa hilo la Gabola linaloongozwa na Askofu Makiti limeanzishwa miezi miwili iliyopita lakini tayari limeshapata waumini 500 na kuwabatiza watu 2000 kwa kutumia pombe ambayo mtu anayebatizwa anaichagua. 


Chanzo: jamiiforums.com






Maoni