KUBEBA MABEGI NDIKO KULIKOSABABISHA KUFANYA VIBAYA MKOA WA DAR ES SALAAM MIAKA ILIYOPITA.

Hayo yamesemwa leo Jumamosi 27 January 2018 na Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Dar es Salaam Ndg. MUSA KILAKALA wakati akiwahutubia UVCCM na wana Chama wa Chama Cha Mapinduzi Kata ya Kunduchi baada ya kumalizika zoezi la usafi.

Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Dar es Salaam alisema tulipoteza majimbo ya KINONDONI, KAWE, TEMEKE, UBUNGO na KIBAMBA kutokana na watu KUBEBA MABEGI.

"Tulikuwa tunapigiwa simu na kupewa maelekezo ya mtu wa kumchagua alafu unapewa pesa sasa wewe bila kumtathmini huyo mtu kwa utendaji kazi wake unaangalia pesa yake hili kwa Mkoa wa Dar es Salaam lifike mwisho" alisema KILAKALA.

"Viongozi watakaochaguliwa wachaguliwe kwa utendaji kazi wao na wala sio pesa" alisema KILAKALA.

"Kwa kuhakikisha hilo linafanikiwa na hatimaye kuyarudisha majimbo yote mikononi mwa CCM Vijana tunasema HATUBEBI MABEGI" alisema KILAKALA.

"Tunaanza na Jimbo la Kinondoni tunalichukua baada ya hapo tunasubiri uchaguzi mkuu wa mwaka 2019 tunachukua Mitaa yote baadaye 2020 tunachukua Majimbo yote ya Mkoa wa Dar es Salaam" alisema KILAKALA.

Mwisho Ndg. KILAKALA aliwataka wana CCM wa Jimbo la Kawe kuwasaidia Jimbo la Kinondoni na hatimaye kuhakikisha ushindi kwa MTULIA unapatikana mapema.

Maoni