MFENESINI YAANZA KUTOA DOZI MSIMU MPYA UVCCM CHAMAZI REDE CUP

Na shabani rapwi, chamazi dar. 

Team ya Mfenesini ya Chamazi jana imewapa raha mashabiki wake kwa kuanza na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Mwembe Bamia ya Chamazi Bamia,katika mchezo wa Uvccm Chamazi Rede Cup,uliopigwa uwanja wa Mfenesini Chamazi. 

Mfenesini ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 21.

Mwembe Bamia walisawazisha bao dakika ya 32.

Kipindi cha pili kilianza kwa Mfenesini kuongeza kasi na kucheza kwa kujiamini na kwa umakini mkubwa na dakika ya 63 wakajipatia goal la pili.

Dakika ya 74 Mfenesini wakaongeza bao la 3.

Hadi mwisho wa mchezo,Mfenesini imeondoka na ushindi wa mabao 3-1 na kuweza kunasa point 3 muhimu za kwanza kabisa katika mashindano hayo.

Matokeo ya michezo ningne zilizopingwa hapo jana.

Mbande Magengeni imepokea kichapo kinene cha mabao 6-0 toka kwa Kisewe Queens uku team ya Mbande Rufu imepata ushindi wa mezani baada ya Kiponza kuingia mitini.

Maoni