MSUFINI HATUBATISHI - BOFU

Baada ya ushindi wa jana wa bao 4-0 dhidi ya Kwa Mkongo Queens kocha wa Msufini Ibrahim Mtumwa Bofu ametamba na kujinasi kuwa ushindi uwo si wa bahati nasibu team yake ipo vizuri zaidi.

Bofu akizungumza na Shabanirapwiblogsport.com ushindi uwo ni salamu tosha kwa team ya Dovya B ambayo nayo jana ilipata ushinda bao 3-0.

"Team yetu imepata ushindi wa bao 4-0 dhidi ya team ya Kwa Mkongo,tulijianda vizuri,tulifanya maandalizi ya muda mrefu,tufanya kambi ya muda mrefu,tumekuwa tukicheza mipira mizuri,wachezaji wangu wapo vizuri,wapo kwenye hali nzuri,wapo kwenye molali nzuri,na ndio maana tumeibuka na ushindi sio bahati, na sio kubatisha na tuna wataadhalisha team zijazo,wiki ijayo tunacheza na Dovya B ivyo wakae vizuri  tumejipanga vizuri, wachezaji wangu wanacheza vizuri wanadaka vizuri,kwaiyo tunatarajia kutoka na ushindi sisi lengo letu ni kubeba ili kombe la kata" amesema Bofu.  

Kwa ushindi uwo Msufini wanapata nafasi ya kuongoza Kundi B wakiwa na point 3 sawa na Dovya B na Mzambarauni ila Msufini anaongoza kwa tofauti ya bao.

Maoni