MWENYEKITI UVCCM TAIFA AMENITUMA KUWAAMBIA VIONGOZI WA KATA ZINGINE ZA WILAYA YA TEMEKE KUIGA MFANO WA KATA YA CHA CHAMAZI -GWANTWA ALEX MWAKIJUNGU.

Jumatatu 22 January 2018.

Maneno hayo yamesemwa jana na mjumbe wa Baraza kuu UVCCM Taifa Ndg. Gwantwa Alex Mwakijungu wakati akizungumza katika kikao cha baraza la vijana Wilaya ya Temeke.

Ndugu Gwantwa alisema UVCCM iliyo chini ya Mwenyekiti KHERI JAMES inahitaji vijana wabunifu, wenye uwezo wa kutatua changamoto za vijana wenzao, wenye uwezo wa kukemea maovu kwenye jamii na wenye uwezo wa kuisimamia kuitekeleza vizuri ilani ya CCM kama wanavyofanya viongozi wa Kata ya Chamazi.

"Nasri Mkalipa kwa kushirikiana na viongozi wengine wa Kata ya Chamazi wanafanya kazi nzuri sana, sio vibaya na Kata zingine mkaiga wanachokifanya" alisema Gwantwa.

"Mwenyekiti wetu wa UVCCM Taifa amenituma kuja kuwaambia viongozi wa Kata zingine muige mazuri yanayofanywa na Kata ya Chamazi" alisema Gwantwa.

"Kwa sifa hizi ninazowapa Kata ya Chamazi kuna wengine wanachukia nawashauri na wao wafanye kazi pia watapewa sifa hizi, hongereni sana Kata ya Chamazi kwa kweli mnafanya kazi nzuri na kuitoa kimasomaso Wilaya ya Temeke na Dar es  Salaam kiujumla" alisema Gwantwa.

Sambamba na hilo aliwataka wajumbe hao wa baraza kuhakikisha wanatatua changamoto za vijana na kuacha kubeba agenda za watu wengine badala ya vijana wanaowaongoza.

Pia Gwantwa alitoa nafasi kwa kiongozi yoyote wa Kata kumpigia simu pindi wanapomuhitaji na sio kupitia kwa watu wengine.

UVCCM CHAMAZI watoa shukran zao. 

Tunashukuru sana kuona jitihada zetu za kuistawisha Jumuiya zinaonekana kwa viongozi wetu wa ngazi ya Taifa kwa pamoja tunasema  Ahsanteni sana.

Pili tunapenda kusema kwamba tupo tayari kushirikiana na Kata yoyote ili kuendeleza Umoja, mshikamano na kuleta ufanisi katika kazi na hatimaye kutatua kero za wananchi jambo litakalopelekea CCM kuendelea kushika dola.

Pia tunashukuru wajumbe wote wa baraza la Wilaya ya Temeke kwa kutupongeza kwa juhudi tunazozifanya na kukubali kuwa nasi bega kwa bega ili kuhakikisha na wao wanakuwa kama sisi.

KUJIFUNZA MEMA SIO DHAMBI

#HatubebiMabegi.
#TukutaneKazini.

Imetolewa na
Najim Nyanza
Katibu Hamasa na Chipukizi Kata ya Chamazi

Maoni