NITAENDELEA NA UTARATIBU HUU - MH.KARATA

Katika kusaidia na kuendeleza michezo kata ya chamazi Mh Diwani, Hemedi Juma Karata leo ametoa jezi kwa kikundi cha MSUFINI.

Huu ni utaratibu wa Mh.Karata kujitolea jezi kwa vikundi vya ukimbiaji maarufu kama Jogngg  kila mwanzo na mwisho wa mwezi,utaratibu uwo ambao ameuanza toka Oct  mwaka jana 2017 na zaidi ya makundi tisa mpaka sasa yamenufaika na msaada huu wa jezi.

Akizungumza wakata wa zoezi la kukabidhi jezi hizo Mh. Karata amempongeza na kumwagia sifa Mwenyekiti wa Uvccm, Nasri Mkalipa kwa juhudi na utendaji kazi wake asa kuwafanya vijana kuwa wamoja na kukipenda Chama Cha Mapinduzi.
"Nikushukuru sana Mwenyekiti wa Uvccm kata ya chamazi,kata kubwa kabisa kabisa tanzania nzima kwa mujibu wa kukumbu za kiserikali,mdogo wangu Nasri unaongoza Uvccm kubwa kuliko kata yeyote tanzania,kata kubwa inayo ongoza katika nchi ya Tanzani Chamazi,kwaiyo niseme niwashukuru wadogo zangu,nipo pamoja na nyinyi,leo tupo pamoja kesho na kwa kadri tutakavyo jaliwa" amesema Mh Karata

Mh diwani akaendelea kumpongeza Mwenyekiti wa Uvccm kwa kujituma na kuwa mbunifu kwani toka achaguliwe hakuviona rakini sasa anaviona na anaamasika na yupo tayali kuwasaidia vijana kwa kadri atakavyo jaliwa. "Nakupa hongera sana ndugu yangu ni mambo ambayo sijawai kuyaona toka nichaguliwe kuwa Diwani 2015 sasaivi nayaona na naamasika kweli kweli  niko na roho yangu nyeupe kwa ajiri ya kushirikiana nanyi,Leo ndugu zetu wa Msufini kuna jezi zao hapa nitawakabizi nawaomba na kuwaasa sana vijana wangu izi jezi kuzitumia vizuri na kuzitunza,na utaratibu huu tutazidi kuendelea nao na sitaishia kwenye jezi tu nina  mipango mikubwa,sitaji niwe mwongeaji sana nataka vitendo viwe mbele zaidi" 
" amesema Mh. Karata.

Aliye vaa jezi ya azam ni mwenyekiti wa UVCCM kata ya chamazi Ndg Nasri Mkalipa akimpongeza Mh Hemedi Juma Karata diwani wa kata ya chamazi kwa kuendelea kuthamini michezo. 

Maoni