SHAKA H SHAKA AIPONGEZA UVCCM KATA YA CHAMAZI KWA KAZI KUBWA WANAYOIFANYA.

Leo tarehe 13/01/2018 kaimu katibu mkuu uvccm taifa NDG. SHAKA HAMDU SHAKA`atoa pongezi kwa viongozi wa uvccm kata ya chamazi kwa kuchapa kazi na kuwa kata ya mfano wa kuigwa```

```pongezi hizo amezitoa Leo baada ya kutoa andiko refu la kuipongeza UVCCM chamazi na kuzitaka sehemu nyingine kuiga Kazi kubwa inayofanywa na viongozi hao```

*Andiko hilo ni Kama ifuatavyo:-*

Mnatupa raha😄😄chamanzi hii ndio UVCCM tuitakayo. Michezo ni afya, hukuongeza mahusiano, kuwatoa katika magenge maovu, kuwafanya wenye utii na nidhamu  lakini ni njia pekee ya kuleta hamasa na vuguvugu katika kuendeleza uhai wa jumuiya na chama kwa ujumla.

Ni matumaini yangu hii itakuwa chachu ya kuwaunganisha vijana baada ya mashindano yenu  kufikiria namna gani mtakaa chini kutafakari katika nyanja za uchumi ili kuwahamasisha vijana wenzenu kutumia fursa mbali mbali zilizopo.

Mumeanza vizuri sana nasi viongozi wenu tuko tayari kuwashika mkono kuwaonyesha njia za kuelekea mafanikio.

Nawapongeza sana UVCCM kata ya Chamanzi mumekuwa mfano na kielelezo kizuri mbele ya vijana wenzetu hasa katika kuunga mkono kauli mbiu ya Mwenyekiti wetu wa CCM  na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Joseph Magufuli  Hapa Kazi tu sambamba na Mwenyekiti wetu wa UVCCM Taifa  Ndugu Kheir D. James  "Tukutane kazini"

Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni narejea tena mnatupa raha Vijana wa Chamanzi ni matumaini yetu matawini, kata  na wilaya zote nchini watajifunza na kuiga mfano mzuri kwa vijana wa CCM Chamanzi.

TUKUTANEKAZINI

```UVCCM kata ya chamazi inatoa shukrani zake za dhati kaimu katibu mkuu Shaka kwa kutambua kazi kubwa inayofanywa UVCCM chamazi na  kuahidi kuzidisha kasi na ari ya hali ya juu ili kuhakikisha ilani ya chama cha Mapinduzi ya awamu hii ya tano inatekelezwa ipasavyo```

IMETOLEWA NA:-
NAJIM NYANZA
KATIBU HAMASA NA CHIPUKIZI
UVCCM CHAMAZI

Maoni