Taarifa ya Redio Kwizera Kuhusu Waandishi wa Habari Kukamatwa wilayani Kahama mkoani Shinyanga.

Padre Damas Missanga amesema taasisi inamtambua mtuhumiwa huyo Bw. Saimoni Dionizi kama mwandishi wa kujitegemea anayeripotia Radio Kwizera kutoka Kahama lakini tuhuma hizo haziihusu taasisi na wala hakutumwa kufanya hivyo.

Padre Missanga ameeleza kwamba Radio Kwizera, kama chombo cha habari kitaendelea kujikita katika maadili ya uandishi wa habari wakati wote, kutoa huduma kwa jamii kwa kuzingatia haki, weledi na sheria za nchi na hivyo inaomba radhi kwa wadau na wasikilizaji wote waliopata usumbufu kutokana na taarifa hiyo.

Katika taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari inaeleza kuwa waandishi wa habari watano wilayani Kahama mkoani Shinyanga wamefikishwa mahakamani kwa makosa ya kujifanya maafisa usalama wa taifa na kujipatia shilingi Milioni 1 kutoka kwa Jane Mbeshi mkazi wa kitongoji cha Ng’wande kata ya Mwaluguli ambaye ni mganga wa jadi.

Waandishi hao ni Paul Kayanda wa gazeti la Uhuru, Raymond Mihayo- Habarileo, Shaban Njia-Jamboleo, Simon Dioniz- Radio Kwizera na George Maziku ambaye hajulikani anaandikia chombo gani.

HAPA CHINI ISOME TAARIFA KAMILI.

Maoni