TANZANIA YAPATA UFADHILI MKUBWA WA MAGONJWA MATATU HATARI.


Tanzania inatazamiwa kufikia malengo yake ya kufikia viwango vya chini vya uwepo maradhi ya Ukimwi, Malaria na Kifua kikuu ifkapo mwaka 2020 baada ya kupata jeki ya zaid trion moja kutoka shirirka la Global fund.
Msaada huo unaotajwa kuwa mkubwa zaidi kutolewa katika mapambano ya maradhi hayo unatazamiwa kusaidia juhudi za serikali ya Tanzania kutokomeza maradhi hayo kama inavyonuwiwa na malengo endelevu ya umoja wa mataifa.
Miongoni Mwa maeneo yatakayonufaika na fedha hizo ni mikoa ya nyanda za juu kusini na maeneo ya Pwani mwa Tanzania ambayo takwimu zinaonyesha maambukizi ya virusi vya Ukimwi bado yako juu.

Maoni