TATU MZUKA WAONGEZA NGUVU MBANDE UJENZI WA KITUO CHA POLISI.

Katibu tawala (W) Temeke ndg Hashim Komba leo tarehe, 10-01-2018 akipokea fedha taslim 5,000,000/- kutoka kwa muwakilishi wa kampuni ya tatu mzuka ambao wanajishughulisha na uchezeshaji wa bahati nasibu

Tatu mzuka wametoa msaada huo kwa ajili ya kuunga mkono ujenzi wa kituo cha polisi daraja 'c' eneo la mbande magengeni Jijini Dar es Salaam ambacho kinajengwa kwa nguvu za wananchi na misaada kutoka kwa wadau mbalimbali.

Akizungumza baada ya upokeaji msaada uwo Komba amehishukuru kampuni iyo ya TATU MZUKA kwa kutoa msaada uwo "Tunawashukuru sana tatu mzuka kuja kutuongezea nguvu kwenye ujenzi huu wa kituo chetu cha polisi,kwa niaba ya wananch wote tunasema asant sana"

Pia akaendelea kwa kusema "Ni vyema makampuni mengine yakainga mfano wa kampuni ya tatu mzuka kwenye kuunga mkono maendeleo kwani kukamilika kwa kituo iki kitakuwa msaada mkubwa sana kwenye ulinzi na usalama wa wananch wengi" alisema  Komba

Maoni