UVCCM CHAMAZI REDE CUP KUANZA KUTIMUA VUMBI JAN 06.

Mashindano ya UVCCM CHAMAZI REDE CUP msimu mpya wa 2017-18 kuanza kutimua vumbia kuanzia kesho jumamosi Jan 06.

Mechi za ufunguzi hiyo kesho MSUFINI watakuwa wenyeji wa MBANDE uwanja wa shule ya msingi Chamazi Jijini Dar es Salaam.

Wageni wa mashindano KWA MKONGO QUEENS watawakaribisha MFENESINI. Kwa mkongo wageni kwenye mashindano aya lakini usajili wao makini na wa gharama kubwa wadau weng wakiwapa nafasi kubwa ya kufanya vizuri zaidi kwenye mashindano ayo.

KISEWE QUEENS wana kibarua kigumu mbele ya SAKU A hii ni mechi ambayo itakuwa na ushindani mkubwa sana kwa pande zote mbili ingwa baada ya wadau na mashabiki wakipa nafasi zaidi kisewe kutokana uchezaji wao na kuwa na wachezaji wengi na wenye uwo wa hali ya juu.

RUFU watakipiga thidi ya MZAMBARAUNI. Rufu ni team ambayo inaonekana bado kuimalika imecheza mechi mbili za kirafiki na zote imepoteza kwa kufungwa goal 3 kwa 0,pia Mzambarauni imecheza mchezo moja ya kirafiki na ikapoteza mchezo uwa kwa kufungwa goal 3 pia kwa 0 unaona izi ni team ambazo zinaweza kuwa na kiwango sawa.

DOVYA B watamenyana na KIPONZA. Kiponza ni team ambayo bado haifanyi vizuri sana rakini naamini kwa usajili na maandalizi walio yafanya wataleta ushindani mkubwa sana.

DOVYA A watafunga panzia la  ufunguzi wa mashindano aya kwa kucheza na BAMIA. Dovya A wamekuwa na kiwango kizuri na team yao kuimaliki kila siku wamecheza mchezo mmoja wa kirafiki walishinda goal 3 kwa 0.

Mechi izo zote zitapigwa majira ya saa 10 jioni kwenye uwanja wa Shule ya msingi Chamazi Jijini Dar es Salaam kwa kila team kucheza dk 20 na mgeni rasm wa ufunguzi uwo ni JOKATE MWEGELO a.k.a KIDOTI.

Maoni