UVCCM CHAMAZI WASHIRIKI IBADA YA MAZISHI YA MAMA MKWE WA DIWANI ALIYEMALIZA MUDA WAKE MH. GAMA.


Leo Alhamisi 4 January 2018 viongozi na wanachama wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Kata ya Chamazi wameshiriki zoezi la kumuaga na kumuombea dua mama Mkwe wa Diwani aliyemaliza muda wake 2010 - 2015 Mh. John Gama.

Ibada hiyo ilifanyika nyumbani kwa Mh. Gama Chamazi, Mfenesini jijini Dar es Salaam.

Akizungumza baada ya Ibada ya  kumuaga marehemu huyo ambaye maiti yake imesafirishwa leo kwenda jijini Mbeya kwa mazishi, Mwenyekiti   wa Idara ya maafa na matukio UVCCM  Kata ya Chamazi Ndg. Ally Yasin Andarus alimpa pole Mh. Gama na kumwambia kuwa UVCCM Chamazi wapo nae katika kipindi cha  shida na raha.

Akizungumza kwa niaba ya familia ya Marehemu Mh. Gama aliwashukuru sana viongozi pamoja na wanachama wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Kata ya Chamazi kwa moyo wao wa huruma na kumkimbilia haraka mara tu walipopata taarifa ya msiba huo.

Pia Umoja huo umemteua Katibu wa UVCCM Tawi la Mfenesini ndugu Elias Matuso kusindikiza msiba huo.

Maoni