Vyakula Vyakuzingatia wakati ukiwa unafanya mazoezi ya kupunguza mafuta mwilini.


Vyakula ni muhimu sana hasa wakati mtu unataka kupungua vema na kuwa na afya,maana walio wengi wana amini unene ndio afya kumbe si kweli. Ni vizuri ukawa na ratiba ya vyakula vya kuzingatia na kujua pia faida zake mwilini sio kula tu ilimradi umekula.Kuna aina mbalimbali ya makundi ya chakula nayo ni kama
1. Wanga (Carbohydrates).
2. Protein.
3. Mafuta (fats and oils).
4. Vitamini (vitamins).
Carbohydrates ni aina ya chakula ambacho ndani yake kina carbon,Hydrogen na oxygen pia kuna sukari na wanga ndani yake (starches) ambavyo hutumika mwilini kutengeneza nguvu(to produce energy) ,Carbohydrates kwa kawaida hupatikana kwenye mimea (plant Sources). Carbohydrates ikiingia mwilini huvunjwavujwa na kutengeneza glucose ambayo ndio hutumika kuupa mwili nguvu. Nguvu mwilini hutumika katika makundi mawili ambayo ni Ndani ya mwili na Nje ya mwili
Ndani ya mwili ni kama Kupumua,Kusukuma damu,Kusaga chakula na kazi nyingine za mwilini.
Nje ya mwili ni kama Kufanya kazi,Kucheza michezo mbalimbali na shughuli zozote zinazohusiha viungo vyako.
Na carbohydrates hii tunaipata kwenye mimea kama,
1. Mboga za majani na matunda
2. Sukari
3. Mchele
4. Ugali na vingine vya mfano wa mimea
5. Spageti
6. Mkate
Protein ina mchanganyiko wa carbon,oxygen,hydrogen and nitrogen,pia protein ina mchanganyiko mkubwa wa Amino acids. Protein hutumiwa na mwilini kufanya kazi zifwatazo
Kusaidia ukuaji na maendeleo ya kila siku ya mwili katika kuujenga.
Kutengeneza body structures kama muscles,tissues na organs including moyo,mapafu,na organs za kusaga chakula.
Kutengeneza Enzymes,kwa mfano zile zinazosaidia kusaga chakula.
Na hormones mbalimbali mwilini.
Kwahiyo ukiangalia utagundua kwamba protein ni muhimu sana mwilini na inaitajika na mwili sana.kwakuwa husaidia kusaga chakula na hata kukuza mwili wako. NB Watoto wadogo wanahitaji sana protein kuliko kitu kingine kwakuwa huwasaidia katika
kukua kwao. Protein hupatikana katika vyakula kama,
1. Nyama (meat)
2. Samaki (Fish)
3. Mayai (Eggs)
4. Karanga na Maharage.
Mafuta(Fats and oils) ni chakula muhimu sana kwani mwili unahitaji fat kila siku kwa afya na kujisikia vizuri kama unavyohitaji vyakula vingine.
Fats inatumika mwilini kwa mambo mengi muhimu kama:
Katika muundo wa chembechembe hai za mwili (cell structure)
Kutengeneza nerves na akili.(the brain is 40% fat)
Kuupa mwili joto
Kutengeneza sex hormones
Kunyonya baadhi ya vitamini kama A,D,E and K
Mafuta (fats and oils) hupatikana kwenye..
1. Animal meat
2. Fish
3. Vegetable oil
4. Parachichi
5. Njugu
Vitamins na Minerals ni vitu ambavyo vinapatikana katika aina mbalimbali ya vyakula,kwahiyo kwa kula vyakula tofauti unaweza kupata vitamins nyingi na minerals za kutosha kwa afya.
Minerals zinafanya mambo mengi sana mwilini ikiwemo kujenga mifupa na meno,kurekebisha mapigo ya moyo na kusafirisha oxygen kutoka kwenye mapafu kwenda kwenye tissues.

Katika makundi yote haya ya chakula niliyo yataja ni muhimu sana kuzingatia na kuhakikisha unapata kila kundi katika mlo wako wa siku,na pia ni vema kuzingatia kiwango unachokula kama nilivyosema katika topic iliyo pita kwamba usipendelee kula sana mpaka usikie tumbo limejaa,bali kula kidogo kidogo kwa nafasi ya masaa mawili mpaka matatu.Pili uzingatie maji yakutosha mwilini penda kujizoesha kunywa maji mara kwa mara na usipende kunywa maji mara tuu baada ya kumaliza kula kwani wataalamu wanasema kwamba maji baridi yanapokwenda tumboni system ya tumbo huanza kuyapooza kwanza maji ili yawe katika joto linalotakiwa kwa ajili ya kuingia kwenye system ya mwili,kwa wakati huo chakula kinakuwa kimesubirishwa kwanza kitu ambacho hakishauriwi kiafya.

Mwisho kabisa ni kuzingatia mazoezi kila asubuhi,najua itakuwa ngumu kwa wanaoanza mara ya kwanza,Ntakuja na topic kuhusu jinsi ya kuanza mara ya kwanza mazoezi( Beginners)
Maana usingizi wa asubuhi si mchezo kama huna malengo inakuwa kazi kweli kweli.

Maoni