WAHUJUMU WA TASAF IRINGA KUCHUKULIWA HATUA.


Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela Amewakata Wanufaika wa Mradi wa Kupunguza Kaya Masikini Nchini wa TASAF Ambao Wameingia Katika Mradi Huo Kimakosa Kujisalimisha Serikalini na Kurejesha Fedha za Mradi Huo.

Wakati wa Mkutano Wake wa Wazi na Wananchi wa Kijiji cha Mfyome Kata ya Kiwele Wilayani Humo, Kasesela Wajanja Wachache Wenye Uwezo wa Kimaisha Wamejipenyeza Katika Mradi Huo wa Kupunguza Kaya Masikini wa TASAF.

Mkuu Huyo wa Wilaya Amesema Serikali Yake Itaanza Kuhakiki Rasmi Orodho na Uhalisia wa Wanufaika wa TASAF Ili Kuwabaini Watu Wanaohusika na Kufifisha Malengo ya Mfuko Huo Unaofadhiliwa wa Serikali na Benki ya Dunia.

Maoni