BARABARA YA KIJIJI CHA IHANGA YASABABISHA WANANCHI KUILILIA SERIKALI

Wananchi wa kijiji cha Ihanga wilayani Makete mkoani Njombe, wamemueleza diwani wao kuwa ahakikishe barabara ya kwenda kijijini hapo inapitika kama zilivyo barabara zingine kwa kuwa wanaonekana kama wametengwa kutokana na barabara hiyo kutotengenezwa kwa muda mrefu.

Katika Mkutano wa hadhara kijijini hapo wananchi hao wamesema, hali ni ngumu katika kijiji hicho kwani wanashindwa kusafirisha mazao yao ama kufuata huduma maeneo ya jirani kwa kuwa barabara hiyo haipitiki hasa msimu huu wa mvua
Akizungumzia hilo Diwani wa kata ya Ukwama Mh Augustino Tweve amesema amekuwa akiibana serikali katika vikao vya baraza la madiwani kuhusu tabu wanayoipata wananchi hao, na kuwaomba kuwa na subira kwa kuwa limeshafikishwa serikalini anaimani litafanyiwa kazi mara moja, na kilio cha wananchi hao kitamalizika.

Chanzo: Greenfm tanzania

Maoni