YALIYOSEMWA NA MKURUGENZI WA MANISPAA YA UBUNGO NDG. JOHN LIPESI KAYOMBO WAKATI WA KIKAO NA WAMILIKI SAMBAMBA NA WAPANGAZI WA MAENEO YA BIASHARA KATIKA MITAA YA MUUNGANO NA TUPENDANE KATA YA MANZESE.



Jumatatu 12 Fabruari  2018.

"Maeneo ya wazi huwa hayabadilishwi matumizi labda kama kuna sababu ya msingi"- Kayombo.

"Sinza kuna water viosk, watu wamejenda kiholela nimepiga X maeneo hayo, kama kuna nyumba , ghorofa katika maeneo hayo nitavunja" - Kayombo.

"Maamuzi ya serikali kwenye hayo maeneo hayo ni kuna wizi na  mikataba yote mliyoingia ni feki kwa maana anayeingia Mkataba ni mmiliki na kwa upande wa Serikali ni Mkurugenzi na Meya" - Kayombo.

"Nyinyi mmehodhi mali miaka yote, hamuoni aibu kuwa Serikali inapoteza mapato?" - Kayombo.

"Ukipitia mikataba hii unaweza kulia kama ni mzalendo kweli, hakuna hata mkataba mmoja wa Mwanasheria" - Kayombo.

"Lazima wananchi ifike sehemu tuisaidie Serikali, kipindi cha kujipatia fedha kiudanganyifu hakipo" - Kayombo.

"Kwa muda huu wapangaji wote wa Mitaa ya Tupendane na Muungano wapo chini ya Manispaa ya Ubungo"- Kayombo.

"Tumeanza na Manzese baada ya uchaguzi tunaenda kubomoa Sinza nilipotia X" - Kayombo.

"Mamlaka zote zinajua kuwa tunarudisha Mali zote serikalini ili ziwasaidie wananchi wote" - Kayombo.

"Hatuwezi kuwa tunakosa madawati wakati nyie mnatuibia, mtu anapata millioni tano wakati hana hati, kajenga katika Mali ya umma, haikubaliki" - Kayombo.

"Nikichukua ramani yangu inasoma open space ( maeneo ya wazi) na hati yako inasema eneo la makazi nafuta, inawezekana uliibiwa" - Kayombo.

"Tunaachana na yote yaliyopita tunaanza upya na naapa maeneo yote ya serikali yatarudi ndani ya Manispaa ya Ubungo labda Mimi niondoke hapa" - Kayombo.

"Baada ya Sinza kubomoa nitatangaza kuuza viwanja hivyo au nitatafuta ubia" - Kayombo.

"Maamuzi haya niliyoyafanya Manzese nitayafanya katika Kata zote" - Kayombo.

"Nawatuma nyinyi mkaawambie na wengine kuwa zoezi hili litafanyika katika Kata zote 14 za Manispaa ya Ubungo" - Kayombo.

"Mapato yote yatakayopatikana katika Mtaa husika yatajulikana katika Mtaa huo na risiti zitakuwa ni za serikali sio za kihunihuni" - Kayombo.

"Kama haujaridhika na maamuzi haya nenda popote, narudia tena kama haujaridhishwa na maamuzi haya nenda popote" - Kayombo.

"Niwashukuru sana kwa kuitikia wito na wale wote wamiliki wasiofika muwaambie kuwa hayo maeneo ni ya serikali na sio yao tena na wapangaji wasiofika muwaambie kuwa kuanzia sasa mmiliki wao ni Serikali" - Kayombo.

"Mwisho niseme wapangaji wote mliopo katika maeneo hayo hakuna atakayewatisha, nyinyi nyote mliopanga mpo chini ya serikali na mtapewa utaratibu mpya na tutapeleka matangazo katika maeneo hayo kuwaambia kuwa maeneo hayo ni ya serikali" -  Kayombo. 
Picha Zote Na Kitengo cha Habari na Uhusiano
Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo. 

Maoni