Boko Haram wachoma kijiji kizima Nigeria,Watu wawii wachomwa wangali hai


Kundi lenye itikadi kali za Kiislam la Boko Haram,jana limechoma kijiji kizima kilichoko Kaskazini Mashariki mwa nchi ya Nigeria,na kuua watu wawili kwa kuwachoma wakiwa hai.

kwa mujibu wa Shirila la habari la AFP,lililowakariri baadhi ya wananchi,na vyanzo vya usalama,Boko Haram,limetekeleza shambulizi hilo katika kijiji cha Alau-Kofa, takribani kilometa 12 sawa na maili 7.5 kutoka maji kuu wa jimbo la Maiduguri,ambao ni makao makuu ya jimbo la Borno.

AFP limedai kuwa kundi hilo limetumia silaha mbalimbali kukiangamiza kijiji hicho ikiwemo maguruneti,na maroketi.

Chanzo : Channel  Tena Tz. 

Maoni