CCM IRINGA MJINI YATEKELEZA AHADI YA SOKO KUU

CHAMA cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Iringa mjini kimetekeleza ahadi ya TV iliyoahidiwa wakati wa kampeni za ubunge mwaka 2015 na mbunge wa jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa (Chadema) katika soko kuu la Manispaa ya Iringa .

Akizungumza leo mara baada ya kukabidhi TV hiyo na king'amuzi chake kwa uongozi wa soko kuu mjini Iringa mwenyekiti wa CCM wilaya ya Iringa mjini Said Rubeya alisema kuwa CCM imelazimika kutekeleza ahadi hiyo ya TV nchi 58 baada ya wafanyabiashara wa soko hilo kuomba kusaidiwa TV hiyo kwa ajili ya kufuatilia habari mbali mbali zinazojiri nchini wakiwa katika sokoni hapo .

Alisema pamoja na kuwanunulia TV hiyo aina ya Sumsung wamepata kuwanunulia king'amuzi pamoja na kuwalipia malipo ya mwezi mmoja kuwa lengo la CCM kufanya hivyo ni kuendelea kuwahudumia wananchi na kutatua kero mbali mbali za wananchi bila kujali itikadi za vyama vyao .

" CCM tumeendelea kutekeleza ahadi mbali mbali ila kama mtakumbuka kata ya Kihesa kulikuwa na jengo ambalo lilikwama kwa zaidi ya miaka 10 ila baada ya CCM kushinda katika uchaguzi mdogo wa kata ya Kihesa mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa (NEC) Salim Abri aliahidi na tayari ametekeleza hivyo CCM tukiahidi tunatekeleza wenzetu wakiahidi wanatelekeza ahadi zao "

Mwenyekiti wa CCM Iringa mjini Said Rubeya kushoto akiwakabidhi wafanyabiashara soko kuu TV na king'amuzi ikiwa ni utekelezaji wa ahadi iliyomshinda mbunge wa jimbo la Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa (chadema) miaka 10 toka ahahidi 

Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati ,katibu wa CCM Iringa mjini Marko Mbanga na mwenyekiti wa CCM Iringa mjini Said Rubeya wakiwa na wafanyabiashara baada ya kutekeleza ahadi iliyomshinda mbunge Msigwa.


Na MatukiodaimaBlog

Maoni