DC HOMERA ADHAMIRIA KUWARUDISHA SHULE WANAFUNZI WENYE ULEMAVU WALIOFAULU NA KUSHINDWA KWENDA SHULE KWA SABABU MBALIMBALI

DC Homera ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilayani Tunduru mkoani Ruvuma amefikia maamuzi hayo wakati wa  kikao cha Tathmini ya Elimu wilayani hapo, 

Aidha DC  Homera alifikia maamuzi hayo baada ya kusomewa taarifa ya watu wenye ulemavu(Viwete) watatu 3 walishindwa kulipoti shuleni msimu wa mwaka 2016/2017 na wengine watano 5 wamefaulu msimu wa 2017/2018 nao kunauwezekano wa wazazi kuacha kuwapeleka shule kwa sababu zisizo za msingi, kwa upande wake DC Homera ameamuru wanafunzi wote wenye ulemavu wa viungo (viwete) wanane 8 wapelekwe  shule mara moja mwaka huu 2018 kwa kwa kugharamiwa na mfuko wa Elimu wilayani Tunduru ikiwemo na kununuliwa wheelchair 6  kwaajili ya wanafunzi wenye ulemavu wa viungo na tayari DC Homera ametafuta wafadhili kwaajili ya kuwawezesha walemavu Wawili ambao walishindwa kwenda shule 2016/2017 ili waende ,hivyo DC Homera aliwakabidhi baiskeli za miguu minne wheelchair kutoka kwa Ndg Victor Mingwe ambaye alijitolea baada ya kuguswa na jambo hilo na ameshamkabidhi mwanafunzi Khadija Rashid Mkota ambaye alitakiwa awe kidato cha pili  mwaka huu katika shule ya sekaondari ya wasichana iringa (Iringa Girls) lakini ilishindikana kutokanana na sababu mbalimbali ikiwemo na mzazi mwenyewe kutokumweka mwanae ambaye ni mlemavi sio kipaumbele katika familia lakini pia walemavu wa ngozi (Albino) jumla yao 29 DC Homera ameagiza wanunuliwe mafuta(lotion),Miwani na kofia kutoka katika mfuko wa Elimu ili waweze kujisomea vizuri.

Maoni