DIAMOND,HAMISA MOBETO WAFUNGA JALADA MATUNZO YA MTOTO

HATIMAYE jalada la kesi ya madai ya matunzo ya mtoto lililofunguliwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu upande wa watoto na Mwanamitindo maarufu nchini, Hamisa Mobeto dhidi ya mwanamuziki, Naseeb Abdull 'Diamond Platinumz' limefungwa rasmi.

Akizunguma leo na waandishi wa habari baada ya kutoka mahakamani Diamond amesema, walifika mahakamani hapo kwa ajili ya kuweka kumbukumbu ili upande wa Ustawi wa Jamii na Mahakama ziwe sawa ili kesho na kesho kutwa kisije kikazungumzwa kitu kingine cha uongo.

"Tunategemea, mtoto wetu aje kuwa mtu fulani ama kiongozi, hivyo nawashauri wazazi wa kiume na wa kike wajitahidi kuweka majivuno yao pembeni wanapokuwa na migogoro na wasimuingize mtoto", amesema Diamond.

Amesema kufanya hivyo kwa namna moja ama nyingine ina muathiri mtoto.
"Nilazima kuweka majivuno pembeni ya matatizo yetu binafsi kwa kuwa yana muumiza mtoto, ni lazima muangalie ni namna gani mnatengeneza mazingira mazuri ya kuweza kumlea na kumsaidia mtoto,"amesema.

Naye, Wakili wa Mobeto, Walter Godluck amesema ustawi wa jamii unasaidia katika usuluhishi wa kesi za watoto ambazo zinahusu malezi ambapo baba na mama wanakubalina ni jinsi gani wanaweza kulea mtoto.

Amesema, leo wameleta ripoti ya usuluhishi mahakamani hapo ambapo kesi ya msingi ya matunzo ya mtoto ilifunguliwa.Amesema, malalamiko waliyoyaleta kuhusu matunzo ya mtoto upande wa pili wameridhia na wameona kuna haja ya kuyafanyia kazi na kwamba kiasi cha fedha walichokubaliana nacho wamekiweka kifamilia.


Wakili huyo amesema wazazi wamekubali kushughulikia malezi ya mtoto, na kuwa Diamond yupo tayari kumlea mtoto na atafanya hivyo kwa uwezo wake .Huku akicheka kuashiria furaha, Hamisa Mobeto amesema" kuhusu maamuzi nimeefurahia nayo, sababu panda zote mbili tulikaa tuka discuss na tukakubaliana nayo, nashukuru kila mtu ameridhia nayo ameridhika nayo na yamekwisha" amesema Mobetto.

Mobeto alifungua kesi ya matunzo ya mtoto mahakamani hapo, pamoja na mambo mengine alikuwa anaiomba Mahakama imwamuru Diamond kutoa matunzo ya mtoto ya kila mwezi.

Kupitia hati hiyo ya madai, Mobeto alikuwa akiiomba Mahakama imuamuru Diamond amuombe msamaha kwa kumsababishia madhara yaliyoishtua familia yake.

Maoni