DIWANI KARATA AWA MGENI RASMI BONANZA LA UPATU LA JOGGING ZA JIMBO LA MBAGALA.

Jumapili 4 February 2018.

Diwani wa Kata ya Chamazi Mh. HEMEDI JUMA KARATA leo Jumapili 4 February 2018 amealikwa na kuwa mgeni rasmi katika bonanza la upatu kwa Jogging za Jimbo la Mbagala lililofanyika Katika Kata ya Chamazi.

Bonanza hilo lililoandaliwa na klabu ya michezo (jogging) ya KWA MSOMA lilihusisha vilabu 20 kutoka maeneo mbalimbali ya jimbo la Mbagala.

Pia Mh. KARATA alikabidhi shillingi 250,000 kwa klabu ya KWA MSOMA kutokana na pesa ya michango kutoka kwa klabu zingine zinazoshiriki upatu huo.

Akizungumza wakati wa bonanza hilo Mh. KARATA alisema michezo ni afya na pia inasaidia kuleta undugu, upendo na mshikamano.

Pia alisema Katika kuhakikisha analeta hamasa kwa vijana ataendelea kutoa jezi kwa klabu zote za Kata ya Chamazi.

"Mpaka sasa nimetoa jezi kwa vilabu saba kikiwemo hiki na katika kuhakikisha naendeleza michezo kwa vijana nitaendelea kutoa kwa vilabu vingine vilivyobaki" alisema KARATA.

"Kwa heshima mliyonipa napenda kuwakabidhi kiasi cha pesa 250,000 kwa klabu ya KWA MSOMA ambazo zimechangwa na klabu zingine kupitia mchezo wenu wa upatu".

Maoni

Chapisha Maoni