Diwani Kata Mabwepande awatolea uvivu Dawasco Bagamoyo.


DIWANI wa Kata ya Mabwepande iliyopo Wilaya ya Kinondoni, Suzan Massawe, amewajia juu dawasco Bagamoyo kutokana na kutoridhishwa na kitendo cha kufunga mita kuu  ya  maji huku wananchi wake wakiendelea kupata shida.


Diwani Suzan Massawe (aliyesimama ), akizungumza na wananchi wa Mtaa wa Mji Mpya Kata ya Mabwepande  katika kuwaelezea hatua mbali mbali anazochukua katika kutatua changamoto ya huduma ya Maji hivi karibuni (PICHA NA YUSUPH MWAMBA)

Akizungumza na Waandishi wa habari leo, Suzani, amesema wana zaidi ya  mwezi huduma ya maji ni changamoto kiasi cha kuwatesa wakazi wa eneo na kuwafanya wakazi hao kutumia maji yasiyo rafiki kwa afya ya binadamu.

Suzan, amesema hali ya wananchi wake ni mbaya, kipindu pindu kimeanza kunyemelea maeneo hayo hii yote ni kutokana na kunywa maji ambayo hayakidhi katika afya ya binadamu.

Aidha, amesema shauri la madai ya malalamiko juu ya kufungwa kwa  mita na dawasco lilifikishwa Ewura , ambapo majibu yaliyotolewa ni kwamba dawasco wafungue mita na wananchi wapate maji kwa gharama ya bili ya milioni 4 kila mwezi kama ilivyo awali.

Lakini baada ya shauri hilo, Dawasco wameonekana kukaidi agizo la Ewura, jambo ambalo linazidi kuwaweka  njia panda na kujua ni nani mwenye mamlaka ya kutoa idhini ya upatikanaji  wa maji.

“Napenda niseme, huu ni ukiukwaji wa haki za bianadamu, wakazi wangu wanateseka, wanashindwa kufua, kuoga na kupika kutokana na ukosefu wa maji, lazima tufike wakati haki hii tuidai kwa nguvu zote hadi kieleweke”,amesema Suzan

“Mradi wa maji, ni kwa ajili ya waathirika wa eneo langu walio kuja hapa , lakini cha kushangaza kuna ujanja ujanja unafanywa wa kuchomekea watumiaji wengine, lakini dawasco wao huu mradi hauwahusu , pale kwenye ungio la maji wameweka mita yao ambayo sio nzuri ina wanyonya wananchi wangu hili ndio chimbuko la tatizo inafikia wakati bili inakuwa kubwa kwa kuwapa mzigo ambao hawastahili kuubeba”,ameeleza zaidi Suzan

Amemtaka Rais John Pombe Magufuli,  kuingilia kati suala hili kwani tayari walishapeleka shauri ya kesi hiyo lakini dana dana zimeonekana kuwa nyingi ,pamoja na kamati ya maji kufanya jitihada bado dawasco wamekiuka agizo la Ewura.


Eneo ambalo Mita ya Maji imefungwa  

Naye, mwenyekiti wa Kamati ya M taa wa Mji Mpya, Joseph Mwampamba, amekiri uwepo wa shauri hilo lakini amesema walalamikiwa ambao ni dawasco wamedai kutofungua mita mpaka deni la mita yao lenye thamani ya milioni 23 limalizike kisha wafungue maji.

“Tunashindwa kuelewa, baada ya kuhamia hapa tulitengeneza kamati kwa mujibu wa sheria, tuliamua kuwa na mita yetu ambayo haitaingiliana na watumiaji wengine,walitufungia mita bila idhini yetu, lakini  wameendelea kushikilia msimamo wa kutumia mita yao kitu ambacho kimeendelea kutuumiza kwani mita waliyoifunga inasoma bila ya pointi wakati yetu inasoma na pointi na gharama yake inakadiria milioni 4 tofauti na yao “,amesema Mwampamba.


Mita ya Maji iliyofungwa na  Dawasco ya Bagamoyo inayolalamikiwa na Wakazi wa Mji Mpya wakidai inawaubia na haitendik haki katika malipo 

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Mtaa wa Mji Mpya, Justine Chiganga, amesema wana mwezi na zaidi tangia bomba hilo lifungwe, lakini ameitolea lawama mita ya dawasco akidai inawaibia wananchi .

Ameupongeza uongozo wa kamati ya maji kwa jitihada za kuleta maji ya boza kama mbadala lakini changamoto ya maji hayo sio rafiki kwa afya za bianadmau wengine wanaugua kipindu pindu, matumbo  na typhoid    shauri ya kutumia maji hayo.

Chiganga, ameiomba Serikali  iwasaidie ili waendelee kupata huduma ya maji huku wakisubiri shauri ya kesi ikifanyiwa kazi ambapo usikilizwaji wake unatarajia kufanyika Februali 21 na 22.

“Hii mita waliyotufungia hawa mabwana sio nzuri, inatuongezea madeni kwa kifupi hatuna imani nayo, hivyo tunaomba turudishiwe mita yetu ya zamani ili haki itendeke maisha magumu halia ya uchumi imekaa vibaya kwa kila mtu”,amesema Chiganga

Mkazi anayeishi Mji Mpya, Tima Mahadhi, amesema wanachokifanya dawasco ni kumchonganisha Rais na wananchi, kwani ilishatolewa eneo na mradi huo wamepewa sasa kama dawasco wanakiuka agizo la Ewura ni sawa na kukiuka kauli za Rais katika jitihada zake za kuona wananchi wake wanapata huduma bora ikiwemo hili la maji safi na salama.


Mtaa wa Mji Mpya uliopo Mabwepande mpaka sasa una zaidi ya wakazi 8000 waliojiandikisha na kuanishwa kwa mujibu wa Diwani wa kata hiyo,  huku wakazi hao wakiwa wanatokea maeneo mbali mbali kama  vile Tabata na Jangwani.

Maoni