DIWANI WA CHAMAZI ACHANGIA NYAMA KILO KUMI KWA AJILI YA VALENTINE DAY.

Leo Jumatano 14 February 2018 (siku ya wapendanao) Diwani wa Kata ya Chamazi Mh. Hemed Karata ameichangia Jumuiya ya Vijana ya Chama Cha Mapinduzi Kata ya Chamazi kilo kumi za nyama ya Ng'ombe.

Kilo hizo kumi ni kwa ajili ya maandalizi ya sherehe ya siku ya wapendanao inayotarajiwa kufanyika leo kuanzia saa kumi kamili jioni.

Sherehe hizo zitakuwa kwa ajili ya kudumisha upendo kati ya viongozi wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi na wanachama wa Umoja huo ambapo itachezwa mechi ya Mpira wa Miguu kati ya mashabiki na wanachama washabiki wa Timu Yanga na Simba.

Pia kutakuwa na zoezi la ugawaji kadi kwa wanachama wapya takribani 500, zoezi ambalo litafanywa na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Wilaya ya Temeke Ndg. 
Fadhil Mohammed (FAMONGA).

Mgeni rasmi katika sherehe hizo zitakazofanyika katika ofisi ya Tawi la CCM Kisewe anatarajiwa kuwa Mstahiki Meya wa Mansipaa ya Temeke Mh. ABDALLAH CHAUREMBO.


Wa kwanza upande wa kushoto ni Mwenyekiti Wa Uvccm kata ya chamazi Ndg. Nasri Mkalipa, wa kati kati ni Diwani Wa kata ya chamazi Ndg. Hemedi Juma Karata na wa mwisho Katibu wa Uvccm kata ya chamazi Ndg. Juma Bega. 
Picha ya na Najim Nyanza. 

Maoni