DIWANI WA KIJICHI AMEPOKEA MABATI 30 KWA AJIRI YA UEZEKAJI WA OFISI YA SERIKALI YA MTAA

Diwani Kata ya Kijichi Mh Eliassa Kassim Mtalawanje leo hii amepokea mchango wa mabati 30 kwa ajiri ya uezekaji wa ofisi ya serikali ya mtaa wa Mission Kijichi kutoka kwa Mjumbe wa Baraza Kuu Taifa UVCCM-Dar es salaam Ndg.Gwantwa Alex Mwakijungu kama njia ya kuhamasisha ushiriki wa wananchi katika kutekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi CCM.


Ndg. Gwantwa Alex alitumia nafasi hiyo kuwashuruku wakazi wa Kijichi kwa niaba ya Umoja wa Vijana CCM Dar es salaam kwa imani kubwa walionyesha kwa Chama Cha Mapinduzi na Vijana kwa kumchagua Mtalawanji kuwa Diwani wa kata hiyo katika uchaguzi mdogo uliofanyika mwishoni mwa mwaka jana.

"Mtalawanje ni Kijana mwenzetu. Kumchagua kwenu nyinyi wananchi wa Kijichi kuwa Diwani wenu ni dhamana ya vijana wote wa UVCCM Dar kwani yeye anatuwakilisha sisi. Utendaji wake ndio mwangaza wa sisi vijana katika duru za uongozi kwani akifanikiwa yeye,sisi tutakuwa na jeuri ya kugombea nafasi nyingine za uwakilishi kwa kumtumia yeye kama mfano wa kuwa Vijana tunaweza. Na nina waahidi kuwa sisi viongozi wa jumuiya tutakuwa nae bega kwa bega kuhakikisha mipango ya maendeleo ya Kijichi inafanikiwa."


Diwani Mtalawanje amemshukuru  Ndg. Alex na kuomba wadau wengine mbalimbali waweze kujitokeza na kutia nguvu katika shughuli za kimaendeleo mbalimbali ili kusaidia kuonesha njia kwa serikali katika kutatua changamoto za raia.

Maoni