Diwani wa KIJICHI azidi kutekeleza Ilani ya CCM

Wananchi wa kata ya Kijichi iliyopo Manispaa ya Temeke  Jijini Dar es salaam,  wamejitokeza kwa wingi katika zoezi la kufanya usafi ikiwa ni juhudi za kuunga mkono jitihada za Rais Magufuli kutaka Tanzania Safi.

Hatu hiyo imefikiwa leo na Diwani wa kata ya kijichi na wananchi wake Mhe.ELIASA MTARAWANJE ikiwa ni moja ya vipaumbele vyake alivyovitaja wakati akiwania kiti cha udiwani wa kata hiyo.

Diwani wa Kata ya KIJICHI akifyeka Msitu katika zoezi la usafi la kila wiki kikata.

"vipaumbele hivi vya usafi pia ni katika kumuunga mkono Rais Magufuli, tunatambua usafi ni jambo ambalo ni Muhimu na lilitangazwa na Mhe Rais Magufuli pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe.Paul Makonda "Amesema Mhe.Eliasa

Mwananchi akifyeka Msitu

Ameendelea kusema kuwa hatua hiyo wanayoifanya ni muhimu sana kiafya na pia kimazingira kutokana na maeneo mengi kuonekana yametelekezwa(Misitu).

"haya maeneo yote ambayo tumeyafyeka leo sio maeneo tu ya serikali ni maeneo ya watu binafsi" . Amesema Mhe.Mtarawanje

Ameeleza, eneo ambalo wamefyeka siku ya leo ni msitu ambao upo karibu na shule kitu ambacho ni hatarishi kwa wanafunzi wanaosoma shuleni hapo ,kwani wenda majambazi wanaweza kutumia kama kichaka cha kufanyia uovu,na hata kuwadhuru Raia.

MO7 NEWS imeshuhudia wananchi wakifanya usafi katika nyumba zao.

Aidha amewaasa wananchi kuendelea kujitokeza kwa wingi pindi inapofika siku hiyo ili kujumuika kwa pamoja kutekeleza azma ya Raisi Magufuli ambayo yeye anaiunga Mkono.

Diwani Mtarawanje amesema kwasasa anakampeni ya "USINICHAFUE KIJICHI INANITEGEMEA" ikiwa na lengo la kuhakikisha kijichi inakuwa safi .

Amesema kata hiyo ni kata ya kipekee katika Manispaa ya TEMEKE na ni kata ambayo imechaguliwa kuwa ya Mfano katika masuala ya usafi hivyo anaendelea kuwahamasisha wananchi kudumisha usafi katika mazingira wanayowazunguka.

Zoezi hilo litaendelea tena wiki ijayo ambapo wafanya usafi katika mtaa wa Mwanamtoti iliyopo kwenye kata hiyo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mtaa huo Bw. yabini Mwinyimvua Amempongeza Mhe Diwani kwa kuonyesha Juhudi zake tangu aingie Madarakani na kuwapa changamoto viongozi waliokuwapo Madarakati tangu zamani na ameahidi kuendelea kushirikiana nae.

"Utaratibu wetu wa kufanya usafi ni kila Jumamosi ya wiki na ile ya mwisho wa mwezi "Amesema Bw.Mwinyi Mvua

Mwenyekiti wa Serikali za Mtaa wa Kijichi Mh Mwinyimvua akizungumza na Waandishi wa Habari.
Nae katibu wa siasa na uenezi katika kata hiyo Bw Mohamed limbanga amesema kwa kiasi kikubwa watu wameweza kujitokeza kufanikisha jambo hilo ambalo ni utekelezaji wa Ahadi ya Mhe Rais Magufuli ambalo linatiliwa mkazo na Diwani huyo.

katibu wa siasa na uenezi katika kata hiyo Bw Mohamed limbanga  akizungumza na vyombo vya Habari.
"Tunamshukuru Mhe.Diwani kwa kuratibu jambo hili vizuri na wananchi wameweza kujitokeza kwa wingi  na sisi kama chama Cha Mapinduzi Tunamshukuru kwa kutekeleza Ilani ya Chama hicho ".Amesema Limbaga

Zoezi hilo la usafi lilipambwa na ufanyaji mazoezi "Jogging"kwa vikundi mbalimbali vya kata hiyo.

Chanzo : Mo7News

Maoni