Dkt Slaa afunguka mengi kuhusu maisha yake katika siasa.

Dkt Slaa anasema gari lake limeshawahi kukamatwa na cocaine tani tano mwaka 1991 na lilikaa polisi miaka 8 ila uzuri alilikodisha kwa kampuni hivyo yeye hakuusishwa. Baada ya hapo aliingia kwenye siasa na anaelezea nafasi alizoshika CHADEMA.

Anasema baada ya hapo watu wanasema ameondoka kwenye siasa, anasema Serena Hotel alisema anaachana na siasa za vyama vingi na active politics, na akaahidi kutokuwa mwanachama wa chama cha siasa na amejiuzulu siasa za vyama.

Amesema, Serena alisema mtu akihitaji jambo la kupigiwa kelele lenye maslahi atalipigia kelele.

Anasema yeye hakusepa wala kufukuzwa kanisa katoliki bali alifata taratibu za kutoka na alipata decree ya kutoka 1998 ndio maana yeye hana tatizo na kanisa katoliki. Ndio maana hata lilipokuja suala la ndoa, anasema ndoa haifungwi na padri bali ndoa inafungwa na wahusika wawili, padri ni ofisa.

Amesema February 2016 alifunga ndoa ya validation kwenye kanisa katoliki, anasema yeye amekuja kwa sababu yeye ni mwenyekiti wa CCBRT na sio mambo ya ubalozi. Amesema nchini kuna mabadiliko mengi na wao CCBRT wameguswa, ilitakiwa kujiandikisha upya na waliandikiwa kuwa wanaweza kufutiwa usajili, sheria iliyotungwa mwaka 2002 na kufanyiwa marekebisho 2015. Hivyo kilichomleta ni mchakato wa kuhamisha usajili wa shirika.

Dkt Slaa anasema Canada ni nchi ambayo ni kama haina mwenyewe, miaka 500 iliyopita watu wengi walihamia, wao wanaona popote ulipotoka, ukifika Canada wewe ni mcanada. Anasema Canada, kazi ni maisha na so msemo kama Tanzania na ndio maana ya maendeleo. Anatolea mfano watu wanavyofika ofisini na kufikia kusoma magazeti karibu saa nzima au kunywa chai.
Anasema nchi ni tajiri na watu pia matajiri na ni kwa sababu wanafanya kazi, pia anasema huduma zote ziko standard.

Dkt Slaa: Balozi siendi kutekeleza sera ya CCM, naenda kutekeleza sera ya taifa. Mambo yakishaingia bungeni na kupitishwa hayawi tena ya CCM, yanakuwa ya taifa. Anatolotea mfano Karatu walivyotekeleza sera ya Taifa kwa namna ya CHADEMA kwa sababu walikuwa na madiwani theluthi mbili.
Slaa anatoleaa mfano walivyomsomea Mkapa sera ya zahanati kila kijiji Karatu na yeye alivyofika akaifanya sera ya taifa kwa zahati kila kijiji. Kuhusu kauli ya Mnyeti kuhusu watendaji wasiounga mkono serikali, itakuwa ni makosa kwani analazimisha.

Kuhusu kadi za CHADEMA na CCM, anasema hakurudisa kadi ya CCM na sheria inasema uanachama unajulikana kwa kadi lakini pia kuonekana kwenye jukwaa la chama kingine unakuwa sio mwanachama. CHADEMA alisema ameondoka lakini kadi ni kumbukumbu yake na ameilipia hivyo ni haki yake.
Amesema mweekeo wa siasa nchini haumfurahishi, anasema baada ya Uhuru kulikuwa na vyama vingi, baadae vikaanza kufa vyenyewe ka sababu vilikatisha tamaa wananchi na baadae vikaondoka kisheria.
Anasema anasikitika kwa sababu ameshiriki kujenga upinzani nchi na haoni chama chenye sera zilizonyooka. Mikakati ya utekelezaji kwa serikali iliyoko madarakani duniani kote ni kipindi cha kutoa ahadi na sera sera mbadala na hakuna mtu anaesema wameiba au wamenyang'anya kwani sera ikitoka hadharani ni za nchi nzima.

Chanzo : Kulunzi Fikra. 

Maoni