ERDOGAN kukutana na PAPA FRANCIS VATICAN,Kujadili masuala kadhaa ikiwemo Jerusalem na Ugaidi


Rais wa Uturuki Rechip Tayep Erdogan,alikuwa anatarajiwa kukutana na kiongozi mkuu wa kanisa katoliki duniani Papa Francis,mjini Vatican,katika ziara ya kwanza kwa kiongozi wa Uturuki kuzuri Vatcan,katika kipindi cha miaka 60.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na ofisi ya bwana Edowan,viongozi hao watajadili hali kuhusu Jerusalem,uhusianao katia ya Uturuki na Vatican na mgogoro wa wakimbizi pamoja na ugaidi.

Papa Francis,ni miongoni mwa viongozi ambao wamekuwa wakipaaza sauti kuhusu hatua ya Rais Donald Trump,kuitambua Jerusalem,kama mji mkuu wa Israel.

Ziara ya mwisho ya mwisho kufanywa na kiongozi wa Uturuki,katika makao makuu ya kanisa katoliki Vatican, ilikuwa mwaka 1959,ambapo zilianzisha uhusiano wa kidiplomasia.

Maoni