GWANTWA ARIDHISHWA NA MAENDELEO YA UJENZI WA OFISI MPYA YA UVCCM KIGAMBONI, YAFIKIA HATUA YA LINTA

Na Shabani Rapwi.

Jumanne 20 February 2018.

Kigamboni, Dar es Salaam.

Mjumbe wa Baraza Kuu UVCCM Taifa Ndg. Gwantwa Alex Mwakijungu jana Fabruary 19 alitembelea Wilaya ya Kigamboni na kushiriki katika ujenzi wa ofisi  ya UVCCM ya Wilaya hiyo na kuridhishwa na Maendeleo ya Ujenzi wa Ofisi hiyo mpya ya UVCCM Kigamboni.

Akizungumza baada ya kushiriki zoezi hilo la ujenzi wa ofisi hiyo Ndg. Gwantwa alisema 

"Leo nimesindikizwa na Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Ilala Ndg. Hamad Pazzi kutembelea hapa wilaya ya Kigamboni na kushiriki katika ujenzi wa ofisi ya UVCCM wilaya"

"Kwa ushirikiano na uongozi wa Jumuiya ya Vijana Wilaya chini ya Bw. Mponela Mathei tayari ujenzi wa ofisi hii umefika kiwango kizuri huku tukitegemea kufunga lenta mapema siku ya jumatano ya tarehe 21/02/2018"

"Nashukuru kwa ushirikiano ninao upata kutoka kwa vijana wenzangu wa Chama waliojitolea kwa hali na mali katika kufanikisha hili wakiongozwa na Q.S Aboubakar Jafo, Architech Prosper William, Bulugu Magege, Hamad na wengine wote ambao muda wao wamejitolea kuhakikisha tunafanikisha kusimamisha ofisi hizi za UVCCM Mkoa wa Dar es salaam"

"Dira hii na lengo hili litafanikiwa kwa mashirikiano kutoka kwa wadadu"  alisema Ndg. Gwantwa Alex Mwakijungu. 



Maoni