KATIBU MKUU TAMISEMI AIONYA HALMASHAURI YA MJI WA BABATI.

Halmashauri ya mji wa Babati imeshauriwa kuchimba visima vya maji katika eneo la Maisaka katani inapotarajiwa kujengwa kwa kituo cha mabasi wakati wanasubiri kupata maji kutoka Darakuta mradi kutoka Mamlaka ya maji safi na usafi wa Mazingira [BAWASA].
Pia imeelezwa kuwa kutoa maji eneo la Darakuta [long plan]lililopo zaidi ya Kilometa 20 kutatumia mabilioni ya pesa.
Ushauri huo umetolewa na katibu mkuu ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa [TAMISEMI] Eng.Mussa Iyombe alipotembelea eneo hilo la Katani na kushuhudia pakiwa na msitu huku kukiwa hakuna dalili yeyote ya kuanza ujenzi.
Mkurugenzi wa mji wa Babati Fortunatus Fwema alieleza mbele ya katibu mkuu kuwa tatizo lililopo katika maeoneo hayo ni kukosa wanunuzi wa viwanja huku Katibu akieleza kuwa hata kama ni yeye asingeweza kununua kiwanja
maeneo hayo ya katani ambayo hayana huduma za maji wala umeme.
Amemtaka mkurugenzi na watumishi wengine kutimiza wajibu wao kwa wakati na sio kulalamika.
Ikumbukwe kuwa kwa sasa Halmashauri ya mji wa Babati haina kituo cha mabasi baada ya kituo kilichopo kukabidhiwa kwa chama cha Mapinduzi.
Kufuatia hatua hiyo Halmashauri imepanga kuanza na kituo cha muda kwa kujenga kibanda kwa ajili ya abiria kufikia na choo huku wakichukua maji kwa gari hatua ambayo katibu amesema ni kufeli.

Maoni