KATIBU UVCCM UBUNGO ATOA UJUMBE MZITO KWA VIJANA NCHI NZIMA.

Katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Ubungo Ndg. Leah D. Mbeke amewataka vijana kutokubeba mabegi.

Ujumbe huo ameutoa Leo baada ya kukipitia na kukisoma kitabu maarufu cha HATUBEBI MABEGI.

Akizungumza baada ya kujipatia nakala ya kitabu hicho Ndugu Leah D. Mbeke aliwaasa vijana kukataa kabisa kubeba mabegi na kufanya kazi za jumuiya bila kushikiwa akili na mtu yoyote.

Akizungumza na mtunzi wa kitabu hicho Ndugu NASRI MKALIPA, Katibu wa UVCCM WILAYA YA UBUNGO NDG. LEAH D. MBEKE alisema.

" Nassir, Ni jambo jema kuaminiwa na kupewa dhamana ya kuwatumikia watu, ila ni jambo baya kutumia imani yao kujinufaisha wewe na kuwasahau wao....usibebe begi la maagizo yaliyo nje na kanuni zetu...maagizo yanatakiwa yaendane na kanuni zetu..hilo begi usibebe mwachie mwenye nalo" alisema Leah D. Mbeke.

"Nashauri vijana nchi nzima wakitafuta na kukisoma kitabu hiki ili kiwakomboe kifikra na mawazo" alisema LEAH D. MBEKE.

Maoni