KATIBU UVCCM WILAYA MKURANGA ANENA MAZITO, KUUSU KATA YA CHAMAZI.

Jumapili 4 February 2018.

Katibu Uvccm wilaya ya Mkuranga, Ndg Hanzurun Mtebwa atoa pongezi kwa Umoja wa vijana wa Ccm kata ya chamazi kwa kazi nzuri wanayo ifanya.

Pia amewataka viongozi watumie nafasi zao ipasavyo pia wasiwe waoga kujifunza kwa mtu/watu walio pata mafanikio kwani kujifunza akuna umri,yoyote anaweza kuwa mwalimu wa mwingne pasipo kujali umri wala rangi.

Pia amesema yuko tayali kwenda chamazi kujifunza na yeye kupata mafanikio kama ilivyo kwenye kata hiyo ya chamazi.

Nukuu ya waraka wake 

"Naomba kuchukua fursa hii kuwapongeza UMOJA WA VIJANA WA CCM Kata ya CHAMAZI kwa kazi nzuri ya Kutimiza  majukumu yao kwa vitendo. Hongereni sana👋🏾

Baada ya pongezi hizo pia naomba  nitumie fursa hii  kwa  kusema nijuavyo mimi nikiamini katika falsafa sahihi kuwa hakuna asiye mwalimu wa mwenzie katika maisha hivyo  kila mmoja anahitaji kujifunza  kwa mwengine hii itakufanya uweze kuwa na wigo mpana wa kuelewa uliyokuwa huyajui kabla.

Na katika kujifunza hakuhitaji umri wa anaepaswa kukufunza  hivyo unachopaswa kujua ni nini unafunzwa.

Na katika Siasa haitaji kuwepo muda mrefu  eti ndiyo kujua zaidi ya aliye chelewa kuwemo

Katika kuamini hilo jiulize Nasir Mkalipa amejiunga lini  CCM na wewe umejiunga lini CCM.

Baada ya Hapo jiulize kwa UHENGA wako umefanya nini CCM na hao wachanga wanafanya nini?

Lakini mimi ni mwenye kuamini  kuwa UHENGA wangu ndani ya CCM hakunifanyi kukamilika bila kupata mengineyo kutoka katika Damu changa

Ninaposema Muhenga ninaisimamia kauli hiyo ni thabiti kwa ajili ya kumbukumbu zangu
Kwakuwa nimesha hudumu kwa nafasi kadhaa ikiwemo Mwenyekiti wa UVCCM KATA

Mwenyekiti wa Wazazi KATA

KATIBU Siasa na  Uenezi  KATA

Sasa ni Miaka kumi ninahudumu katika nafasi ya UKATIBU UVCCM WILAYA
yatoaha kuwa  Muhenga

Kwa minajili hiyo mi ni miongoni mwa wanaCCM niliyeamua kwa dhati ya moyo wangu kuelekea Chamazi kujifunza katika kata hiyo na kuyapeleka katika Wilaya ninayoitumikia kwa sasa

Na ninashukuru ombi langu limekubaliwa na Uongozi wa UVCCM kata kupitia kwa mwenyekiti wao.

Na kama yupo atakeona kujifunza kwa wadogo ni kujishusha basi acha nijishushe ili nijue nisichokijua.

Ninachoweza kuwakumbusha kuwa
HATA MTUNZI NGULI WA VITABU  UREJEA KUSOMA MAANDIKO YAKE ILI AWEZE KUFUNDISHA

Nami naamini katika hilo

Mwisho!
#TWENDENI CHAMAZI TUKAJIFUNZE

HANZURUN  MTEBWA
Katibu UVCCM WILAYA
MKURANGA
04/02/2018"

Maoni