KATIBU WA DIWANI KATA YA CHAMAZI NDG SAID P KUTIA NGUVU MASHINDANO YA UVCCM CHAMAZI REDE CUP 2018.

KATIBU wa diwani kata ya chamazi Said Paul (Said P) jana Februari 16, 2018 amechangia pesa ya usafiri Team ya Rede ya Mbande Magengeni ambayo inashiriki Mashindo ya UVCCM CHAMAZI REDE CUP 2018 na kuahidi kutoa Mipira kwa team hiyo.

Akizungumza na team hiyo Said P amesema.

"Nawapongeza sana kwa kuendela kufanya vizuri kwenye mashindano hayo ya rede cup na pia nawaomba kuendelea kudumisha amani na nidham katika michezo yote iliyobaki na kutoa ushilikiano kwa viongozi wenu "

"Leo nimekuja hapa kuwatembelea katika team yenu na kuunga mkono juudi kubwa wanazo zifanya viongozi hasa katika  swala zima la michezo katika kata yetu ya chamazi pia jana nilikuwa naongea na kiongozi wenu na aliniambia kuwa jumapili mnaenda kucheza Mfenesini na aliniambia kuwa mmekwama kwenye swala zima la usafiri "

"nikiwa kama Katibu wa Diwani nitachangia hiyo pesa ya usafiri kwenda na kurudi na pia nitawapatia  katoni mbili za maji,na waahidi kuwapatia mipira miwili ivyo nipende kumwangiza Katibu wenu Hamasa,Jumatatu aje kuifata Mipira hiyo Ofisi ya Diwani" amesema Said P.

"niwatakie maandalizi mema  kuelekea mchezo wenu dhidi ya mfenesini"

Kwa upende wake Katibu Hamasa wa tawi ilo la Mbande Magengeni Mohammed Omary Mohammed (Adedi) amemshukuru Said P kwa mchango wake huo na amewataka viongozi wengine kuiga mfano wa Katibu huyo. 

Adedi pia aliwataka vijana asa wa Chama cha Mapinduzi kuwa mfano wa kuingwa kuwaheshima viongozi pasipo kujali rangi,dini ama kabila.

Adedi pia aliwataka vijana asa wa Chama cha Mapinduzi kuwa mfano wa kuingwa kuwaheshima viongozi pasipo kujali rangi,dini ama kabila.

 

Wa kati ni Katibu wa Diwani kata ya chamazi Ndg Said P akiwa na anashudia Mazoezi ya team hiyo ya Mbande Magengeni. 

Wachezaji wa Mbande Magengeni wakiwa wanacheza Rede. 

Katibu wa Diwani kata ya chamazi Ndg Said P Akizungumza na wachezaji wa team ya Mbande Magengeni. Wa

Wachezaji wa Mbande Magengeni wakiwa makini wakiwa wana msikiliza Katibu wa Diwani kata ya chamazi Ndg  Said P. 

Katibu Hamasa tawi la Mbande Magengeni Adedi Akizungumza jambo kwa team yake. 

Katibu Hamasa Adedi akipokea kiasi cha fedha toka kwa Katibu wa Diwani kata ya chamazi Ndg Said P. 


Picha zote na shabani rapwi. 

Maoni