KIMBUNGA CHA NDG. POLEPOLE CHA ONDOKA NA OFISI YA CHADEMA KATA YA SONONI ARUSHA MJINI.

21/2/2018.

Viongozi wote wa Chadema wa Kata ya Sononi   Arusha Mjini, wakiongozwa na Gabriel  Simbile  ambaye alikua ni  Mwenyekiti wa Chadema Kata ya Sononi  na Massawe Zabroni Kitomaro aliyekuwa Katibu Mwenezi Chadema katika Kata hiyo wamejivua uanachama wa Chadema na kujiunga na CCM leo.

Aidha kundi kubwa la wanachama wa Chadema wakiongozwa  aliyekuwa Naibu Meya wa Arusha  Jiji  Bwana Msofe wameachana na
Chama hicho na kujiunga na CCM.

Viongozi na Wanachama hao wamepokelewa na Ndg.  Humphrey Polepole akiwa kwenye ziara ya kukagua na kufuatilia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2015 - 2020 Wilaya ya Arusha Mjini.

Maoni